Dai gavana Mandago amewatia hofu wapiga kura

Jackson Mandago

Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago. Picha/JARED NYATAYA 

Na MWANGI MUIRURI

Imepakiwa - Saturday, January 7  2017 at  18:47

Kwa Mukhtasari

Muungano wa wapiga kura kutoka Mlima Kenya wanaoishi katika Kaunti ya Uasin Gishu sasa wanamtaka gavana wao Bw Jackson Mandago ajifunze kuthibiti hisia zake dhidi yao.

 

MUUNGANO wa wapiga kura kutoka Mlima Kenya wanaoishi katika Kaunti ya Uasin Gishu sasa wanamtaka gavana wao Bw Jackson Mandago ajifunze
kuthibiti hisia zake dhidi yao.

“Huyu gavana ni mfano mwema wa muundaji taharuki. Matamshi yake ya ukali na pia misimamo yake halisi ya kikabila ndiyo tishio kubwa kwa
uthabiti wa Kaunti hii. Anateta kuwa tunaelezea wasiwasi wetu kuhusu usalama wetu katika uchaguzi. Aelewe kuwa hofu yetu kuu ni siasa zake yeye mwenyewe,” akasema Bw Moses Ndwiga, mkazi.

Bw Mandago Ijumaa alinukuliwa akisema kuwa kuna wakazi wa eneo hilo ambao kila uchaguzi ukikaribia huwa wanafunga virago na kuelekea makwao Mlima Kenya “na kusambaza propaganda kuwa kuna taharuki ya vita.”

Akasema: “Ninyi mlio na tabia hiyo nawaambia mkome kabisa. Ikiwa Kaunti hii imewahifadhi kwa miaka mitano mfululizo siku moja tu ya
kupiga kura ndiyo inawafanya mhame? Cha kughadhabisha ni kuwa mnaelekea kupigia kura zenu huko kwnu lakini mnarudi hapa baada ya uchaguzi kutupigia makelele.”

Bw Mandago aliwataka hao wajisajili kama wapiga kura wa eneo hilo na wapige kura pamona na wenzao wazaliwa wa Kaunti hiyo.

Akiongea na mtandao wa Swahilihub kwa simu, Bw Ndwiga ambaye ni katibu mkuu katika muungano huo alisema kuwa “gavana huyu huwa na
weledi wa kutumia lugha fiche kutuangazia kama wasiofaa kuwa katika Kaunti hiyo.”

Akisema kuwa Kaunti hiyo ni moja ya zile zilizoathirika vibaya na ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007, Bw Ndwiga alisema kuchaguliwa kwa Bw Mandago kulionekana kama kungesaidia uthabiti wa amani lakini kile kimejitokeza ni kubakia kwa taharuki.

“Ukimsikiza kwa undani, Bw Mandago ako na ujumbe mmoja tu: Kuwa sisi wengine tujiunge na wa kutoka asili ya lugha ya Mandago kumpigia kura.
Anatulazimisha na unajua kunai le kasumba kuwa sisi ndio huhatarisha 'ukiritimba' wa wazaliwa wa Uasin Gishu kuafikia malengo yao ya
kikabila,” akasema.

Uchunguzi

Alisema kuwa Bw Mandago hahitaji uchunguzi wa kina kumuelewa kwa kuwa matamshi yake huwa wazi kama kijitabu kilichowachwa kimefunguliwa
kisomeke na wote.

“Ametwambia kuwa Malaya wa uasin Gishu ni wa kutoka jamii yetu Mlima Kenya. Ametwambia kuwa hatuna budi ila kumuunga mkono Naibu wa rais Bw William Ruto 2022 kama alivyoahidiwa na rais Uhuru Kenyatta. Ameonekana akiongoza maandamano ya kupinga chuo cha jamii yao kuongozwa na asiye wa jamii yao,” akasema.