http://www.swahilihub.com/image/view/-/4564474/medRes/1974678/-/9hrjp9z/-/dwewa.jpg

 

RAIS ATAKIWA KUTIA SAINI MSWADA WA KULINDA HAKI YA AKINA MAMA KUWANYONYESHA WANAO POPOTE PALE

Julia Njoki

Julia Njoki kutoka Mathare amnyonyesha bintiye mwenye umri wa miezi minane Mei 15, 2018, baadhi ya wanawake walipoandamana baada ya mwanamke mmoja kudai kwamba alifukuzwa hotelini Olive kwa kunyonyesha mwanawe. Picha/CHARLES WASONGA 

Na CHARLES WASONGA

Imepakiwa - Wednesday, May 16  2018 at  12:10

Kwa Muhtasari

Rais Uhuru Kenyatta ametakiwa kutia saini mswada wa sheria kuwapa fursa na ruhusa ama kubainisha wazi wanawake wanaweza kunyonyesha watoto wao katika maeneo ya umma bila vikwazo vyovyote.

 

RAIS Uhuru Kenyatta ametakiwa kutia saini mswada wa sheria kuwapa fursa na ruhusa ama kubainisha wazi wanawake wanaweza kunyonyesha watoto wao katika maeneo ya umma bila vikwazo vyovyote.

Mswada huo ambao ulidhaminiwa na Mbunge Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Murang’a Bi Sabina Chege pia unasema ni sharti waajiri watenge maeneo maalumu kwa wanawake wanyonyesha watoto wao wakiwa kazini, kwa angalau dakika 40.

Wito huu ulitolewa Jumanne na kundi la wanawake waliofanya maandamano katika barabara za jiji la Nairobi kuonyesha ghadhabu yao kutokana na kisa cha juzi ambapo mama mmoja alikatazwa kumnyonyesha mwanawe ndani ya mkahawa mmoja.

Waandamanaji la waliushutumu usimamizi wa mkahawa huo kwa jina Olive Restaurant ulioko katika barabara ya Accra kwa kuhujumu haki ya watoto ambao wanahitaji kunyonyeshwa kwa miezi sita mfulilizo ili apate afya bora.

“Ni aibu kwmba watu wengine au mikahawa inaendeleza vitendo vinavyokiuka haki za watoto kunyonyeshwa. Huu ni unyama ambao haifai kuendelezwa katika jamii ya sasa na tunaupinga kabisa,” akasema Bw Mildred Owiso ambaye ni mwanachama cha Shirika la Kenya Association of Breastfeeding Mums.

“Hii ndio maana tunamtaka Rais Uhuru Kenyatta kutia saini Mswada unaotetea unyonyeshaji (BreastFeeding Bill) uliopitishwa bungeni mwaka jana ili akina mama waruhusiwe kunyonyesha katika maeneo yote ya umma bila vikwazo. Tunasema hivyo kwa hili ni suala la haki ya kibinafsi na afya ya mtoto mdogo,” akaongeza alipohutubia wanahabari nje ya majengo ya bunge.

Kugonga vichwa

Suala hilo liligonga vichwa vya vyombo vya habari wiki jana baada ya mwanamke aliyejitambulisha kama Betty Kim kuweka ujumbe katika mtandao wa Facebook alilalamika kinyanyaswa katika mkahawa huo wa Olive Restaurant. Alisema mmoja wa wahudumu wa mkahawa huo walimwamuru kwenda kumnyonyesha mwanawe chooni wala sio mahala ambapo wateja huketi.

“Nimekasirishwa na Olive Restaurant kwa kunidhulumu nilipokuwa nikimnyonyesha mwanangu. Wahudumu wanafaa kufahamu kuwa ni haki ya mtoto kunyonyeshwa. Ni kinyume cha maadili ya kibindamu kwa wahudumu kunifurusha na kuniambia nikanyonyeshe chooni ilhali mvua ilikuwa ikinyesha,” akaandika Betty.

Usimamizi wa mkahawa huo, ulioomba msamaha na kumtaka mlalamishi kuwajitokeza ili awasaidie kumtambua mhudumu huyo aliyemdhulumu ili achukuliwe hatua za kinidhamu.

“Tunaomba msamaha kwa dhati na tunakuhakikishia kwamba usimamizi wa Olive unafanya kila iwezalo kushughulikia suala hilo. Tafadhali, wasiliana nasi na ikiwezekana utusaidie katika uchunguzi wetu ili tuweze kuimarisha huduma zetu kwa akina mama wengine,” Meneja wa mkahawa huo Moses Wambua alisema.

Jumanne akina mama hao, wengine wakiwa wamebeba wao, walianza maandamano katika eneo la Freedom Corner katika bustani ya Uhuru na kuandamana hadi majengo ya Bunge kabla ya kufululiza hadi nje ya mkahawa wa Olive Restaurant kuwasilisha kero zao.

“Tunataka serikali ya kaunti ya Nairobi na serikali ya kitaifa kuhakikisha kuwa sheria zote zinazotetea haki ya akina mama kuwanyonyesha wanao zitekelezwa haraka iwezekanavyo,” akasema Bi Wanjeri Njeru.

Mbunge wa Gilgil Bi Martha Wangare na Seneta Maalum Isaac Mwaura walijitokeza kupokea taarifa yenye malalamishi ya wanawake hao.

“Shida sio sheria kwa sababu tuna sheria za kutosha zinahimiza unyonyeshaji wa watoto katika maeneo ya umma. Kile tunahitaji na kuhakikisha kuwa sheria hizo zinatekelezwa,” akasema Bi Wangare.

Bw Mwaura aliitaka serikali kuongeza likizo ya akina baba ambao wake zao wamejifungua kutoka miezi miwili hadi miezi sita “ili wanaume wapate muda wa kutosha kusaidia na wake wao kuwatunza watoto wao.