http://www.swahilihub.com/image/view/-/4929388/medRes/2220416/-/ns9syaz/-/skana.jpg

 

Hospitali ya rufaa ya Busia kupokea vifaa vya CT scan

CT Scan

Jengo litakalowekwa vifaa vya kisasa vya CT Scan katika hospitali ya rufaa ya Busia likiwa katika hatua za ukarabati. Picha/GAITANO PESSA 

Na GAITANO PESSA

Imepakiwa - Thursday, January 10  2019 at  15:48

Kwa Muhtasari

Mkuu wa maswala ya afya katika hospitali ya rufaa ya Busia, Maureen Wandera amesema huduma za Computed Tomography (CT) Scan zitaanza mara ujenzi wa jumba la shughuli hiyo utakapokamilika; kipindi chini ya miezi miwili ijayo.

 

BUSIA, Kenya

HOSPITALI ya rufaa ya Busia hivi karibuni itapokea vifaa vya kisasa vinavyoimarisha picha za tofauti za eksirei maarufu Computed Tomography (CT) Scan, hatua mbayo inalenga kupunguza visa vya wagonjwa kutafuta huduma hiyo mjini Kisumu na Eldoret.

Mkuu wa maswala ya afya katika hospitali hiyo Maureen Wandera ameambia Swahili Hub kuwa ukarabati wa jumba litakalotumika kwa shughuli hizo za litakuwa tayari kwa kipindi cha miezi miwili ijayo.

“Baada ya vifaa hivi kuwekwa, hospitali ya rufaa ya Busia itakuwa mojawapo ya vituo vya afya nchini vinavyotoa hudumu hii muhimu adimu kutumia teknolojia ya kisasa,” amesema Bi Wandera.

Huduma nyingine zinazopatikana katika hospitali hiyo hadi kufikia sasa ni pamoja ile ya eksirei, Magnetic Resonance Imaging (MRI), Ultrasound, na Mammography.