http://www.swahilihub.com/image/view/-/3064574/medRes/430606/-/bqm8op/-/Waititu.jpg

 

Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa Kiambu kupata huduma za AI bila malipo

Ferdinand

Ferdinand Waititu. Picha/MAKTABA 

Na SAMMY WAWERU

Imepakiwa - Thursday, January 31  2019 at  12:30

Kwa Muhtasari

Gavana Ferdinand Waititu amesema kila mfugaji wa ng'ombe wa maziwa Kiambu atapata huduma za uhamilishaji (AI) bila malipo.

 

NAIROBI, Kenya

GAVANA wa Kaunti ya Kiambu, Ferdinand Waititu amesema mpango huu unalenga kuimarisha uzalishaji wa maziwa katika kaunti hiyo.

"Kila mfugaji na mkulima aliye na ng'ombe wa maziwa atapata mbegu ya AI bila malipo kuanzia mwezi huu," akasema Bw Waititu.

Alisema mpango huu utagharimu zaidi ya Sh30 milioni, na kwamba tayari pikipiki zitakazosafirisha wataalamu wa huduma hii zimetolewa. Gavana huyyu alisema hayo Jumatano usiku katika mahojiano na runinga ya Citizen kipindi cha JKL.

AI ni njia bora ya uzalishaji wa teknolojia inayoboresha mifugo. Kiambu ni mojawapo ya kaunti zenye kampuni tajika za maziwa nchini kama Brookside na Githunguri, pamoja na wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kisasa. 

Kaunti ya Taita Taveta chini ya gavana wake Granton Samboja mwaka uliopita alitangaza kuwa kila mfugaji wa ng'ombe wa maziwa atakuwa akipata huduma za AI kwa Sh500 kila ng'ombe.

Samboja alisema hilo lililenga kuimarisha sekta ya ufugaji, hasa uzalishaji wa maziwa. Mwaka wa 2016, Nyeri pia ilianza kutoa huduma hizi kwa bei nafuu. Gharama ya huduma hii nchini huwa kati ya Sh1,000-Sh4,000.