http://www.swahilihub.com/image/view/-/4957064/medRes/2237168/-/tb5ubc/-/ikikitu.jpg

 

Mbunge apendekeza mabasi yatakayoletwa yawe faafu kwa walemavu

Denitah Ghati

Mbunge maalum Denitah Ghati. Picha/CHARLES WASONGA 

Na CHARLES WASONGA

Imepakiwa - Tuesday, January 29  2019 at  18:26

Kwa Muhtasari

Walemavu hutaabika sana.

 

NAIROBI, Kenya

MBUNGE maalum Denitah Ghati ameitaka serikali kuhakikisha kuwa mabasi mapya uchukuzi wa abiria ambayo yatazinduliwa jijini Nairobi Februari 2019 yana sehemu maalum za kuwawezesha walemavu kupanda na kushuka kwa urahisi.

Akiwahutubia wanahabari Jumanne katika majengo ya bunge Nairobi, Bi Ghati, ambaye huwaakilisha walemavu bungeni, pia aliitaka Wizara ya Uchukuzi kuhakikisha kuwa mabasi hayo yana sehemu maalum ya walemavu kuketi.

"Watu wanaoishi na ulemavu humu nchini, na haswa  walioko Nairobi na maeneo ya karibu  wamechangamkia mpango wa Wizara ya Uchukuzi wa kuanzisha mabasi makubwa ya uchukuzi wa abiria jijini Nairobi. Lakini tunamtaka Waziri James Macharia kuhakikisha kuwa mabasi hayo yameundwa kwa namna ambapo walemavu wataweza kuyatumia bila matatizo,” akasema huku akiitaka serikali ya kaunti ya Nairobi kujenga vituo maalum vya mabasi vyenye miundo msingi ya kutumiwa na walemavu.

Mnamo Jumatatu Waziri Macharia alitangaza kuwa awamu ya kwanza ya mabasi 64 yatawasilisha nchini mapema Februari na yatahudumu jijini Nairobi.

Alisema mabasi hayo ya kuwabeba abiria wengi yananuiwa kupunguza kero ya msongomano katikati mwa jijini.

Kutatizika

Bi Ghati alisema kuwa mabasi hayo pia yanapaswa kuwafaidi walemavu ambao wamekuwa wakitatizika pakubwa wanaposafiri kwa mabasi ya kawaida ambayo hayana sehemu maalumu ya wao kutumia.

“Hii ndio maana walemavu wengi huwa hushindwa kusafiri kutoka mitaani hadi katikati mwa jiji kwa kutoweza kupanda na kushuka kwa urahisi. Huu ni ubaguzi wa kiwango cha juu kwa walemavu,” akaema