http://www.swahilihub.com/image/view/-/2997314/medRes/1202545/-/11l3nin/-/BDLWED7%25282%2529.jpg

 

Ni marufuku kuhudumu bodaboda baada ya saa tano usiku Uasin Gishu

Pikipiki

Pikipiki. Picha/HISANI  

Na MWANGI MUIRURI

Imepakiwa - Friday, January 11  2019 at  12:34

Kwa Muhtasari

Ni hatua ambayo inalenga kukabiliana na visa vya kudorora kwa hali ya usalama.

 

UASIN GISHU, Kenya

KAMISHNA wa Kaunti ya Uasin Gishu, Abdi Hassan amepiga marufuku uchukuzi wa bodaboda katika Kaunti hiyo, kuanzia saa tano usiku.

Ameteta kuwa habari zote za ujasusi kuhusu ujambazi unaokita mizizi katika Kaunti hiyo masaa ya usiku huwa zinaangazia kuhusika kwa pikipiki ya uchukuzi wa umma.

“Hii ni amri kwa maafisa wote wa kiusalama katika Kaunti hii waanze kufanya kazi yao. Saa tano usiku ndiyo saa ya walevi wawe juu ya usafiri wa bodaboda (kwa wale wanaotumia uchukuzi huu) wakielekea makwao,” akasema.

Akiwa Mjini Eldoret katika uhamasisho kuhusu msimamo huo kwa wadau, alisema kuwa wahudumu hao wa bodaboda watapewa tu dakika kidogo kuanzia saa tano usiku za kujipanga hapa na pale na kisha misako rasmi iwe ikizinduliwa.

“Unajua sisi ni wazuri sana tunawapa ilani kwanza na tunawapa yale masharti ya kutiliwa maanani. Sisi hatuna shida yoyote na wafanyabiashara katika sekta hii ya uchukuzi. Lakini hata ninyi wenyewe mnajua vizuri kuhusu visa vya ukatili mnavyotekelezewa mkipokonywa pikipiki zenu usiku,” akasema.

Bw Hassan alisema kuwa serikali huwa na jukumu rahisi la kulinda waktu na mali zao na katika kufanya hivyo, haitoi mielekeo kwa nia mbaya bali ni ya kuzingatia usalama umedumishwa.

“Hatuko kwa vita na bodaboda au na wahudumu wazo. In fact (Kwa kweli), sisi tunawaheshimu sana kuwaona mkishiriki ujenzi wa taifa hili kwa njia moja au nyingine. Lakini uhalifu ukianza kukita mizizi ndani ya baadhi yenu, hamuwasemi na hamutilii maanani usalama wa kimsingi kuhusu mioyo yenu kama wahudumu, tutawapanga,” akasema.

Alisema kuwa kuahirishwa kwa utekelezaji wa sheria mpya za kudhibitki sekta ya bodaboda hadi Machi 2019 sio msingi wa kusema usalama wa kitaifa au wa Kaunti kwanza pia uahirishwe ukingoja sekta ya bodaboda ipangwe.

“Hapana, sisi tutawapanga kwa kila njia ikiwa kwa udadisi wetu tumegundua kuwa usalama wa wengine wote uko taabani kwa msingi wa harakati moja au baadhi ya wengine katika sekta yoylote ile. Hata tukidadisi tuone shida iko ndani ya maafisa wetu wa usalama, nitaamrisha hata hao wakora ndani yetu wasakamwe,” akasema.