http://www.swahilihub.com/image/view/-/4926080/medRes/2218425/-/4eoot2z/-/kihuta.jpg

 

Mbwa mwitu wafanya uharibifu mkubwa Sikarira

Mbwa mwitu

Mbwa mwitu. Picha/MAKTABA 

Na GAITANO PESSA

Imepakiwa - Tuesday, January 8  2019 at  13:44

Kwa Muhtasari

Wakazi wa Sikarira wilayani Butula wanaishi kwa hofu baada ya mbwa mwitu kuvamia kijiji chao kutoka msitu jirani wa Khareka na hata kuua mifugo.

 

BUSIA, Kenya

WAKAZI wa Sikarira wilayani Butula wanaishi kwa hofu baada ya mbwa mwitu (jackal) kuvamia kijiji chao kutoka msitu jirani wa Khareka.

Mwanakijiji Patrick Opiyo ameambia Swahili Hub kuwa wanyama hao ambao wamekuwa wakirandaranda eneo hilo tayari wamewaua kondoo na mbuzi 10 katika kipindi cha majuma mawili.

“Siku chache zilizopita wanyama hawa walimshambulia mtoto wa miaka miwili na kumjeruhi vibaya. Baadhi ya familia zimesalia manyumbani kwa kuhofia usalama wao,” amesema kupitia mahojiano ya simu.

Wanakijiji sasa wanataka idara ya huduma kwa wanyamapori (KWS) kuchukua hatua za dharura na kuwakamata wanyama hao ili kuzuia hasara zaidi na kuwaondolea wakazi hofu.

“Tunaiomba KWS kushughulikia suala hili mara moja kabla ya kusubiri hadi msiba utufike ama mifugo wetu kushambuliwa,” ameongeza Fredrick Otieno aliyedai kuwa amewapoteza kondoo wake watatu.

Aidha, ameitaka serikali ya kaunti na ile ya kitaifa kuingilia kati na kumaliza uhasama kati ya wanyama wa porini na binadamu katika eneo hilo.