http://www.swahilihub.com/image/view/-/4186722/medRes/1809463/-/4yhso4/-/kai.jpg

 

Mtihani wa mafuriko wakati wa mtihani Kenyatta Girls

Kenyatta Girls

Wanafunzi wa shule ya upili ya Kenyatta Girls' mjini Thika wasafirishwa hadi shuleni mwao ili wafanye mtihani wao wa KCSE 2017. Picha/LAWRENCE ONGARO 

Na LAWRENCE ONGARO

Imepakiwa - Tuesday, November 14  2017 at  17:38

Kwa Muhtasari

Huku mvua kubwa ikizidi kunyesha kote nchini Wasichana wa Kenyatta Girls walilazimika kubebwa na gari la serikali baada ya kukwama barabarani wakienda kufanya mtihani wa kidato cha nne (KCSE).

 

HUKU mvua kubwa ikizidi kunyesha kote nchini Wasichana wa Kenyatta Girls walilazimika kubebwa na gari la serikali baada ya kukwama barabarani wakienda kufanya mtihani wa kidato cha nne (KCSE).

Naibu wa Kamishna wa Kaunti ya Thika Magharibi Bw Tom Anjere na afisa wa Polisi Benard Ayoo walifanya juhudi kuona ya kwamba wanafunzi hao wanasafirishwa kutoka kwao ili wafanye mtihani.
"Nilipigiwa simu na maafisa wa usalama kuwa wanafunzi fulani walikuwa wamekwama katika  maeneo fulani na walihitaji usaidizi wa usafiri haraka iwezekanavyo," alisema Bw Anjere.

Alisema zaidi ya wanafunzi 80 walipewa usaidizi wa gari za serikali ili waweze kufika  katika madarasa yao ya mitihani.

"Mvua hiyo imekuwa nzuri lakini imenyesha kupita kiasi na hata kuleta madhara  kadha  kote nchini," alisema Bw Anjere na kuongeza wananchi hawafai kuchukulia jambo hilo kwa mzaha kwani wako tayari kukabiliana na mafuriko yanayoshuhudiwa kila mahali.

Alisema changamoto kubwa katika tukio hilo la mvua ni kwamba mvua hiyo huja na masaibu yake kwani magonjwa ya Homa ya Matumbo na malaria ziko juu sana .
Alimpongeza mwalimu mkuu wa shule hiyo ya wasichana kwa kuchukua hatua  ya haraka kwa kuarifu serikali kuhusu masaibu ya wanafunzi hao.
Mwalimu  mkuu wa shule hiyo ya Kenyatta, Bi Jane Wambui King'ang'i, alipongeza serikali na wale wote waliojitolea mhanga kuona ya kwamba  wanafunzi wanakalia mitihani yao bila shida yoyote.

"Ninaipongeza serikali na washika dau wote walioingilia kati kuona ya kwamba wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Kenyatta wanapewa usafiri wa dharura ili waende kufanya mtihani," alisema Bi King'ang'i

Siku chache zilizopita mvua kubwa iliyonyesha Gatundu Kaskazini ililazimisha maafisa wa elimu kufikisha makaratasi ya mitihani mapema kabla ya saa 11 alfajiri ili kukabiliana na changamoto ya mvua hiyo.

Alitoa wito kwa serikali kuwa macho na kuhakikisha kuwa shule zinazopitia changamoto za usafiri zinapewa usaidizi haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wasikose kufanya mtihani.

Shule ya upili ya Kenyatta Girls imesajili wanafunzi 152 ambao wanafanya mtihani huo wa KCSE 2017.