Mwekezaji alaumu KeNHA kufanya ubomoaji 'bila kuhusisha umma'

Na MAGDALENE WANJA

Imepakiwa - Wednesday, February 14  2018 at  06:09

Kwa Muhtasari

Mmoja wa wawekezaji waliothirika na ubomoaji unaoendelea katika barabara ya Nakuru-Kabarak ametishia kuishtaki mamlaka ya barabara kuu nchini (KeNHA) kwa kutekeleza ubomoaji huo kinyume na sheria.

 

MMOJA wa wawekezaji waliothirika na ubomoaji unaoendelea katika barabara ya Nakuru-Kabarak ametishia kuishtaki mamlaka ya barabara kuu nchini (KenHa) kwa kutekeleza ubomoaji huo kinyume na sheria.

Bw Herman Kirika ambaye ni mhandisi alisema kuwa kulingana na ramani, ambayo ilitumika katika ujenzi wa barabara hiyo, mamlaka hiyo imevuka mpaka uliowekwa wa upanuzi wa barabara.

Alilalamika kuwa hakuna ilani ilitolewa kabla ya hatua ya kubomoa kuafikiwa.

“Kama mamlaka hiyo iliamua kuongezea kipande cha ardhi cha upanuzi wa barabara hiyo, ilifaa kuwajulisha watakaoathirika pamoja na kuwalipa fidia,” alisema Bw Kirika.

Afisa wa Uhusiano Mwema wa mamlaka hiyo Bw Charles Njogu alisema kuwa walihusisha umma kabla ya ubomoaji huo kuanza.

Alisema kuwa wenye nyumba ambazo zimewekwa alama nyekundu wanatakiwa kuzibomoa nyumba zao wafanye hivyo haraka iwezekenavyo.

“Shuguli hiyo itaendelea kama ilivyopangwa na iwapo walioathirika hawatafanya Hivyo itatulazimu kubomoa sisi wenyewe,” alisema Bw Njogu.