http://www.swahilihub.com/image/view/-/4185830/medRes/1808783/-/yh2304z/-/gaha.jpg

 

Kahiga: Serikali kuu itoe mwongozo kamili wa elimu ya bure sekondari

Mutahi Kahiga

Gavana Mutahi Kahiga wa Nyeri ala kiapo cha kuingia rasmi ofisini Novemba 13, 2017. Picha/JOSEPH KANYI 

Na MWANGI MUIRURI

Imepakiwa - Thursday, December 7  2017 at  07:24

Kwa Muhtasari

Gavana wa Nyeri, Mutahi Kahiga, ameitaka Wizara ya Elimu itoe mwongozo wa karo itakayotozwa na shule zote za sekondari kuanzia Januari 2018.

 

GAVANA wa Nyeri, Mutahi Kahiga, ameitaka Wizara ya Elimu itoe mwongozo wa karo itakayotozwa na shule zote za sekondari kuanzia Januari 2018.

Amesema kuwa hadi sasa habari kuwa serikali kuu itagharamia elimu hiyo kuanzia Januari 2018 hazieleweki vyema na huenda wazazi wengi wajipate wamechanganyikiwa.

“Ukiahidi watu za bure, huwa wanajisahau na ikiwa hilo halitakuwa la kuafikiwa kwa asilimia 100, basi wengi watajipata katika mahangaiko na watoto wao Januari,” amesema Kahiga.

Akiongea katika eneo la Chaka Jumatano, gavana huyo amesema kuwa kile kinahitajika ni serikali kuchapisha mwongozo kamili wa gharama za elimu hiyo na wahamasishwe kuhusu mchango wao wa ufadhili.

“Mwongozo huo useme waziwazi karo itakuwa namna gani Januari, ni kwa kiwango gani mzazi atajipata akigharamia na muundo ambao utatumika kufadhili kwa elimu hiyo,” amesema

Kahiga amesema kuna haja kubwa wazazi wa shule za sekondari za kibinafsi waelewe kama watanufaika na sera hiyo, kwa kiwango gani na walimu wa sekondari wapewe mwongozo wa kujiingiza katika gharama za kufadhjiliwa na wazazi watakuwa wakizingatia nini.