http://www.swahilihub.com/image/view/-/3958360/medRes/1662574/-/japxug/-/SOK.jpg

 

Mwanamume ashtaki duka kwa kujeruhiwa akipigania unga wa Sh90

GOK'

Alama ya 'GOK' kwenye pakiti ya unga wa mahindi wa kilo mbili. PICHA/ LEONARD ONYANGO 

Na SHAABAN MAKOKHA

Imepakiwa - Monday, June 19  2017 at  06:59

Kwa Mukhtasari

MWANAMUME wa miaka 44 katika Kaunti ya Kakamega amelishtaki duka moja la jumla baada ya wahudumu wake kumjeruhi kwenye mafarakano ya kung’ang’ania unga ya bei rahisi mjini Mumias.

 

Bw Jackton Odhiambo, ambaye ni baba ya watoto sita alidai kwamba alishambuliwa na wafanyakazi wa Duka la Jumla la Frankmart, ambapo alipata majeraha mabaya katika kifua na mgongoni.

“Nilikuwa na Sh100 nilipoenda katika duka hilo kununua unga wa kilo mbili kwa Sh90. Hata hivyo, mhudumu mmoja alikataa kuniuzia akisema kwamba lazima ninunue bidhaa nyingine ndipo niruhusiwe kuuziwa unga huo,” akasema Bw Odhiambo.

Alisema kwamba alikuwa na Sh100 pekee na alitaka kununua unga huo ndipo aipelekee familia yake. Alisema kwamba walikuwa wamelala usiku uliotangulia bila chakula, ila rai zake zilipuuziliwa mbali na mhudumu huyo.

Alisema kwamba aliwaomba kuzingatia hali yake, ila meneja wa duka hilo, Bw Pancras Weringo akakataa. Alieleza kwamba aliwaagiza wahudumu wake kurejesha unga huo.

“Nilikataa kuurejesha unga huo, ila wakanigeukia. Nilisisitiza kwamba ni haki yangu kununua unga kama wateja wengine. Hata hivyo, walianza kunipiga,” akasema.

Alieleza kwamba walimfungia katika chumba kimoja kwa karibu saa mbili, ambapo baadaye walimwachilia, ila bila unga huo.