http://www.swahilihub.com/image/view/-/3509896/thumbnail/1529423/-/2n769bz/-/gesaa.jpg

 

Washindi 12 wa Lotto 6/36 watunukiwa Sh1m kila mmoja

Esther Wanjiru

Esther Wanjiru kutoka Kiambu, mshindi wa Sh1 milioni katika shindano la Lotto 6/36. Picha/SAMMY KIMATU 

Na SAMMY KIMATU

Imepakiwa - Sunday, January 8  2017 at  12:35

Kwa Mukhtasari

Watu 12 ni mamilionea baada ya kila mmoja kujishindia Sh1 milioni katika shindano la Lotto 6/36.

 

WATU 12 ni mamilionea baada ya kila mmoja kujishindia Sh1 milioni katika shindano la Lotto 6/36.
Aidha, washindi hao wanatoka katika kaunti 12 fofauti ambapo miongoni mwao walikuwa ni wanajeshi wawili wa KDF, walimu na wafanyabiashara.

Shindano hilo huandaliwa na Shirika la Bahati Nasibu Nchini (KCS)

Meneja wa uhusiano mwema wa shirika hilo, Bw Peter Njoroge aliwakabidhi hundi washindi hao Jumamosi.

Alikuwa ameambatana na meneja msimamizi Bi Jennifer Kilonzo katika hafla ya kuwatuza washindi iliyofanyika katika hoteli ya Meridian, Kaunti ya Nairobi.

Kando na kutunukiwa pesa hizo washindi hao waliandaliwa mlo pia kwenye hoteli hiyo.

Washindi walikuwa ni Bw John Gitau kutoka Mau Narok, Daicy Kirui wa Bomet, Clement Wanga wa Teso Kusini, Samuel Maina kutoka Nyahururu, Desmond Mwenda wa Meru na Kipkemoi Sigei kutoka Kericho.

Wengine ni Richard Langat wa Kericho, Esther Wanjiru kutoka Kiambu, Joseph Njuguna kutoka Kirinyaga, Kuria Kairu wa Mombasa, Kunjal Shah kutoka Nairobi na Paul Ngumbau kutoka Makueni.

Wengi wao walisema ushindi huo umefika wakati mwafaka ndiposa watatumia hela zao kulipia wanao karo shuleni na vyuoni na wengine wanunue ploti wajenge nyumba za kukodisha na kupanua biashara.