Kiongozi wa waasi DR Congo kuwekewa vikwazo

Sultani Makenga

Kanali Sultani Makenga, ambaye ndiye mkuu wa waasi wa M23. Picha/GAAKI KIGAMBO 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Thursday, November 15  2012 at  10:38

Kwa Mukhtasari

Wakuu wa Umoja wa Mataifa na Amerika wameamuru vikwazo viwekwe dhidi ya kiongozi wa kundi la waasi wa M23 wanaopinga serikali nchini DR Congo.

 

WASHINGTON, Amerika

WAKUU wa Umoja wa Mataifa (UM) na Amerika wameamuru vikwazo viwekwe dhidi ya kiongozi wa kundi la waasi wanaotuhumiwa kutekeleza ghasia katika eneo ambalo liko chini yake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

UM uliamuru kuwa Sultani Makenga kiongozi wa waasi wa M23, ambaye anatuhumiwa kwa mauaji na unajisi wa raia, asiruhusiwe kusafiri na mali yake itwaliwe huku ukujaribu kuunda himaya ndogo ndani ya taifa hilo la Afrika  lenye utajiri mkubwa wa madini.

Serikali ya Marekani nayo iliamuru kutwaliwa kwa mali ya Makenya iliyoko Marekani na ikiwakata wananchi wake kushirikiana kwa njia yoyote na kiongozi huyo ambaye alikuwa kanali katika jeshi la Congo. Balozi wa Amerika katika UM Susan Rice alimtaja Makenya kama “katili mbaya zaidi”.

 

 

ZILIZOSOMWA SANA

Uhuru arudi kwa kishindo kutoka ICC

Rais Uhuru Kenyatta alirudi nchini kwa kishindo kutoka jijini Hague ambako alihudhuria kikao cha

MCAs wa Makueni wapitisha hoja ya kumtimua Kibwana

Bunge la Kaunti ya Makueni limepitisha hoja ya kuondolewa kwa Gavana Kivutha Kibwana mamlakani.

Raila ashambuliwa kwa bakora mkutanoni Kwale

Kizaazaa kilizuka leo katika mkutano wa Cord eneo la Kinango kaunti ya Kwale baada ya mwanamume

Raila amtaka Ruto aseme anatoa wapi pesa za harambee

Kinara wa muungano wa Cord Raila Odinga amemtaka Naibu Rais William Ruto awaambie Wakenya