http://www.swahilihub.com/image/view/-/2026776/medRes/597319/-/juilvpz/-/206789-01-02.jpg

 

Maafisa wakuu wapinga ombi la Snowden kutaka msamaha

Edward Snowden

Bw Edward Snowden. Picha/AFP 

Na AFP

Imepakiwa - Monday, November 4  2013 at  13:28

Kwa Muhtasari

Afisa mkuu katika White House na wabunge kadha wa Amerika, wamepinga ombi la Edward Snowden, aliyefichua habari za kijasusi, kutaka msamaha.

 

WASHINGTON,

AFISA mkuu katika White House na wabunge kadha wa Amerika, Jumapili walipinga ombi la Edward Snowden, aliyefichua habari za kijasusi, kutaka msamaha.

Mshauri wa White House Dan Pfeiffer na wakii wa Seneti ya Amerika pamoja na kamati za bunge kuhusu ujasusi walizungumza siku chache tu baada ya mbunge wa Ujerumani kuchapisha barua kutoka Snowden, iliyosema yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya bunge kufafanua uwezekano wa kuwepo kwa hatia kubwa.

“Bw Snowden alikiuka sheria za Amerika,” Pfeiffer aliambia kituo cha televisheni cha ABC.