http://www.swahilihub.com/image/view/-/4567588/medRes/1976739/-/82bne5z/-/luk+pc.jpg

 

Lukuvi ‘aapa kufa’ na waliochagiza mgogoro wa ardhi

 

Na Filbert Rweyemamu

Imepakiwa - Friday, May 18  2018 at  08:12

Kwa Muhtasari

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema atawachukulia hatua za kisheria watumishi wa wizara hiyo waliosababisha mgogoro wa mpaka, kati ya wilaya za Kiteto mkoani Manyara na Kilindi, Tanga uliodumu kwa miaka 22.

 

Kiteto. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema atawachukulia hatua za kisheria watumishi wa wizara hiyo waliosababisha mgogoro wa mpaka, kati ya wilaya za Kiteto mkoani Manyara na Kilindi, Tanga uliodumu kwa miaka 22.

Akizungumza jana na wananchi kwenye mpaka wa wilaya hizo, Lukuvi alisema Serikali imebaini makosa mengi yaliyofanywa na wataalamu wa kusoma ramani waliokuwa wakitumwa mara kwa mara kutatua mgogoro huo.

Akitoa uaamuzi wa Serikali baada ya kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyefanya ziara eneo hilo Januari 18, 2017, alisema matangazo yote ya Serikali yaliyotolewa kuhusu mpaka huo yamefutwa isipokuwa tangazo namba 65 la mwaka 1961 ambalo litafanyiwa marekebisho baada ya kuweka mipaka upya.

Naye Waziri Tamisemi, Seleman Jaffo aliyembatana na Lukuvi, alisema Serikali imedhamiria kuwatumikia wananchi na kuwataka kukomesha migogoro isiyokuwa na tija.

Wengine waliohudhuria ni mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na mwenzake wa Tanga, Martine Shigela.