http://www.swahilihub.com/image/view/-/4660580/medRes/2039882/-/ymik7e/-/may.png

 

May kutoa sababu ya nchi yake kujitoa EU

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May  

Na May kutoa sababu ya nchi yake kujitoa EU

Imepakiwa - Friday, July 13  2018 at  09:54

Kwa Muhtasari

Itaorodhesha maazimio kuhusu eneo la biashara huru, EU


 

London, Uingereza. Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amesema anachapisha maelezo ya mwongozo wake uliosubiriwa kwa muda mrefu wa kuanzisha tena mazungumzo na Umoja wa Ulaya juu ya nchi yake kujiondoa kwenye umoja huo inayofahamika kama Brexit.

Hatua hiyo inakuja baada ya kukabiliwa na uasi mkubwa kutoka kwa mawaziri wanaotilia shaka sera za Ulaya ambao huenda bado ukamuondoa madarakani.

Kwenye taarifa hiyo serikali itaorodhesha maazimio kuhusu eneo la biashara huru pamoja na Umoja wa Ulaya baada ya shinikizo kutoka kwa wafanyabiashara ya kuruhusu biashara ya nchi na nchi kuendelea kama kawaida.

Hata hivyo, Uingereza bado ina mipango ya kuachana na ushuru wa forodha na soko la pamoja. Waziri mpya wa Brexit, Dominic Raab amesema watahakikisha wanakuwa na uhusiano na Umoja wa Ulaya lakini kwa kuzingatia matakwa yao.