http://www.swahilihub.com/image/view/-/4883598/medRes/2190334/-/9awe7t/-/harusi.jpg

 

China yazuia harusi

Bwana na Bibi harusi wakimwagiwa maua wakati wa kuingia ukumbini 

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Thursday, December 6  2018 at  11:31

Kwa Muhtasari

Harusi za sasa ni mfano wa “mwendelezo wa ibada za fedha.”

 

Beijing, China. Serikali ya China imechukua uamuzi unaolenga harusi, ikitaka yafanyike “mageuzi kamili” kuhusu ongezeko la harusi zinazofanywa kwa gharama kubwa.

Wizara ya masuala ya kiraia ndiyo imetoa wito ikitaka kukomeshwa kwa “mazoea ya ndoa za kifahari” kama vile kutoa zawadi ghali, sherehe za kuvutia, na hitaji la mahari kubwa kwa ajili ya bibi harusi - fedha zinazolipwa familia ya wazazi wa mwanamke.

Tangazo la serikali

Katika mkutano juu ya mageuzi ya harusi, maofisa kutoka wizarani walisema harusi zinapaswa “kuakisi vizuri zaidi” maadili na malengo ya nchi na kutekeleza “Fikra za Rais Xi Jinping,” itikadi ya rais kisiasa iliyosifiwa sana. Maofisa hao walisema harusi za sasa ni mfano wa “mwendelezo wa ibada za fedha.”

Tangazo hilo inaelekea limetaka kulenga maeneo ya vijijini, ambako gharama za harusi zimepaa katika miongo miwili iliyopita.

Viongozi walisema viongozi wa serikali wa ngazi za chini na kamati za mitaa ambazo zinaendesha harusi na mazishi katika maeneo ya vijijini zitaombwa kusimamia na kuja na “taratibu za ndoa zenye adabu nzuri”.