http://www.swahilihub.com/image/view/-/4218262/medRes/1829882/-/fxoiunz/-/ramaphosa.jpg

 

Cyril Ramaphosa sasa akaribia kumrithi Zuma

Cyril Ramaphosa

Makamu wa Rais nchini Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ahutubia umma uliojumuika Novemba 13, 2017 katika ukumbi wa Orlando jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Thursday, December 7  2017 at  11:12

Kwa Mukhtasari

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaelekea kupata uungwaji mkono kuelekea mkutano mkuu wa chama tawala cha ANC kupata kiongozi mpya.

 

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

MAKAMU wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anaelekea kupata uungwaji mkono kuelekea mkutano mkuu wa chama tawala cha ANC kupata kiongozi mpya.

Mkutano huu utafanyika kuanzia Desemba 16 hadi 20 jijini Johannesburg na atakayeshinda nafasi ya uenyekiti ndiye atakayesimama kama mgombea wa ANC katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka 2019.

Mpinzani wa Ramaphosa ni aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Nkosaza Dlamini Zuma.

Ramaphosa kwa jumla ameungwa mkono na wajumbe 1,859 huku Nkosazana akiungwa mkono na wajumbe 1,330.

Wengine wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na Spika wa Bunge, Baika Mbete na Waziri katika Ofisi ya Rais Jeff Redebe.

Wawili hao wanaonekana kama wageni ndani ya ANC.

Mapema Novemba, Ramaphosa aliwaambia wafuasi wake kuwa uongozi mbaya umeighrimu ANC na uchumi wa nchi hiyo likiwa kama ‘dongo’ kwa uonozi wa Rais Zuma.

Aliwataka wafuasi wake kubadilisha hali hiyo katika uchaguzi wa chama na akaahidi kukijenga upya na kusimamia miiko ya chama cha ANC.

Hayo yanajiri wakati ambapo Zuma anaendelea kukabiliwa na shutuma zaidi za ufisadi unaohusisha pia familia ya kitajiri ya Gupta.

Rais Zuma anakamiliha muhula wake wa mwisho madarakani mwaka kesho kutwa.