http://www.swahilihub.com/image/view/-/4369558/medRes/1927556/-/12v66ab/-/tshisekedi.jpg

 

EU, AU wampa Baraka zote Rais Mteule Tshisekedi

Mwanawe Tshisekedi ateuliwa kuwania urais DRC

Felix Tshisekedi. Picha/MAKTABA 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Thursday, January 24  2019 at  09:25

Kwa Muhtasari

  • Marekani nayo imeshatambua ushindi wa Felix Tshisekedi wa UDPS

  • Rais anayeondoka Joseph Kabila katika hotuba yake ya kwanza kwa taifa baada ya matokeo rasmi kutangazwa amesema ni muhimu raia wa DRC kuwa na mshikamano

  • Rais mteule wa DRC Felix Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa leo Alhamisi mchana

 

BRUSSELS, Ubelgiji

UMOJA wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika(AU) wametangaza kwamba wametambua hatua ya Mahakama ya Katiba ya kumtangaza Felix Tshisekedi kuwa Rais wa Kidemokrasia ya Jamhuri ya Congo baada ya kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) mshindi wa uchaguzi wa Desemba 30 mwaka jana.

Viongozi hao walisema kwamba wapo tayari kushirikiana na kiongozi huyo mteule anayetarajiwa kuapishwa leo Kinshasa sherehe ambazo zinatarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa mpira mjini hapo.

Viongozi hao wa EU na AU walisema wamejadiliana kuhusu matokeo ya uchaguzi huo katika mkutano wao mjini Brussels, wakidokeza kuhusu uungaji mkono wa mahakama kwa Tshisekedi.

Maofisa hao hawakusema wazi hadharani kwamba wanamtambua Tshisekedi kama mshindi, na hata hawakumpongeza.

Sera

Mkuu wa Sera za Mambo ya Nje wa EU, Federica Mogherini akiwa pamoja na wajumbe wa AU alisema kuwa changamoto zinazomsubiri rais mpya wa Congo ni nyingi katika masuala mbalimbali na yote hayo yanamhitaji awe nguvu ya kuunganisha.

“Rais huyo anatarajiwa kukabili changamoto za uchumi, ulinzi, kijamii na utawala bora’’alisema Mogherini

“Haya yote ni kwamba kiongozi huyo anatarajiwa kukabiliana nayo kwa pamoja ikiwa ni kutoka nje ya nchi kuonana na watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa na wataalamu wa uchumi,” alisema.