http://www.swahilihub.com/image/view/-/4936012/medRes/2224648/-/xbhs57/-/ikiki.jpg

 

Google yawakera wabunge Uingereza

Google

Nembo za kampuni ya huduma za kiteknolojia ya Google katika picha hii ya Novemba 20, 2017. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Tuesday, January 15  2019 at  14:38

Kwa Muhtasari

Yapo matangazo ya mtandao wa Google yanayohamasisha watoto kutozingatia umuhimu wa matamshi ya maneno.

 

BAADHI ya wabunge nchini Uingereza, wamekerwa na matangazo ya mtandao wa Google yanayohamasisha watoto kutozingatia umuhimu wa matamshi ya maneno.

Wabunge hao wamesema matangazao ya mtandao wa Google yanawapotosha watoto kuwa hawana ulazima wa kuzingatia matamshi ya maneno na kuwa ujumbe wa tangazo hilo unajenga utegemezi wa watoto kwenye mitandao.

Walisema teknolojia hiyo inatakiwa kupingwa kwa kuwajengea watoto utamaduni wa kutegemea mtandao wa Intaneti na kuwa hicho ni kiwango kikubwa cha teknolojia ambacho matokeo yake ni kuleta aibu na kuwa unapingana na njia za kukuza elimu.

Mbunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya elimu Robert Halfon alisema teknolojia hiyo imeambatana na tamaa za mtandao wa Google kwa kujaribu kuwashawishi watoto kuwa hakuna ulazima wa kujifunza matamshi ya maneno na badala yake watumie mtandao huo.

Anasema kinachofanywa na mtandao huo ni jambo ambalo sio sahihi na linaleta aibu na kushauri mtandao huo kuwahimiza na kuwajengea uwezo watoto kutamka maneno kwa usahihi bila kutegemea teknolojia hiyo.

Mbunge Mathayo Warman anasema hakuna usawa uliopo katika jambo hilo na kuwa pamoja na kuwa teknolojia ya intaneti inaweza kuwa msaada lakini inatakiwa iwafanye kuwa watu wema na wenye busara na sio wajinga.