http://www.swahilihub.com/image/view/-/4939326/medRes/2226405/-/36w147z/-/ikikila.jpg

 

Ulfat Abdul-Azizi: Kiswahili lugha adhimu

Ulfat Abdul-Azizi

Mkurufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sumait Chukwani Zanzibar, Ulfat Abdul-Azizi. Picha/HAJI MTUMWA 

Na MUHAMMED KHAMIS, Mwananchi

Imepakiwa - Thursday, January 17  2019 at  13:58

Kwa Muhtasari

Mkurufunzi kutoka chuo kikuu cha Sumait Chukwani Zanzibar, Ulfat Abdul-Azizi anataka wadau kujizatiti kuona lugha ya Kiswahili inastawi.

 

VISIWANI ZANZIBAR

MKURUFUNZI kutoka chuo kikuu cha Sumait Chukwani Zanzibar, Ulfat Abdul-Azizi amesema ipo haja mikakati zaidi kuongezwa ili lugha ya Kiswahili iweze kukua na kuenea ulimwenguni kote.

Ameyasema hayo jana Jumatano wakati akizungumza na Swahili Hub mjini Unguja.

“Kwa kiasi fulani Kiswahili kinapiga hatua ingawa ipo haja mikakati zaidi kuongezwa ili kifike mbali zaidi,” akasema Ulfat Abdul-Azizi.

Amesema licha ya kuwa Zanzibar na Tanzania ni watumiaji wazuri wa lugha ya Kiswahili, lakini bado kuna changamoto ambazo anaamini zinahitaji kufanyiwa kazi.

Ametaja changamoto hizo kuwa ni kukosekana kwa mtaala wa kufundishia kwa lugua ya Kiswahili hususani katika ngazi za elimu ya juu; jambo ambalo alisema ni changamoto.

Ngazi ya vyuo vikuu

Ameeleza kuwa ili lugha hiyo izidi kuonekana bora na kuwanufaisha walio wengi, ipo haja pia kutumika kufundishia katika ngazi ya vyuo vikuu.

Mwanaharakati wa lugha ya Kiswahili visiwani hapa, Kauthar Is-hak, amesema Kiswahili ni lugha adhimu ambayo inahitaji kutukuzwa kila leo.

Amesema haipendezi kuona wazawa wanapenda zaidi kutumia lugha ya kiengereza kuliko kutumia lugha mama ambayo ni asili yao.