Magufuli awapa rungu wenyeviti na makatibu wa CCM

John Magufuli

Mwenyekiti wa CCM, John Magufuli akiwahutubia wenyeviti, makatibu wa mikoa na wilaya wa Chama cha Mapinduzi wakati wa kufunga semina  katika Ukumbi wa Ikulu Dodoma Machi 14, 2017. PICHA/ MWANANCHI 

Na HABEL CHIDAWALI

Imepakiwa - Wednesday, March 15  2017 at  15:18

Kwa Mukhtasari

Dodoma, TANZANIA

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) rais John Magufuli amewaagiza wenyeviti na makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya wa chama hicho kuacha urasimu na kufanya kazi kwa manufaa ya wanachama.

 

Alisema hayo Jumanne alipofunga semina ya siku mbili kwa  viongozihao akiwapa rungu la kuisimamia Serikali na hasa watendaji wake.

Habari kutoka kwa wajumbe waliohudhuria semina hiyo zimesema kuwa Rais Magufuli amewataka  kupambana na rushwa  wakati wa uchaguzindani ya chama hicho ili  kuwezesha kuptikna kwa viongozi wasafi na wenye sifa nnakufanya kazi  ya kukirudisha chama hicho kwa wanachama ili kiendelee kupendwa na kuaminiwa na wa kada ya chini.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dl Abdallah Juma Sadala alisema  maagizo ya mwenyekitiwao yalilengga kuwasimamia watendaji na wanachama ili kujua kinachofanywa na Serikali.

Dk Sadala alisema kwa sasa CCM imezaliwa upya  na itaendelea kuwa imara  na imejipanga kwambinu mbadala za kufanya kazi ndani ya chama hicho.

“Ukweli ni kwamba hatuwezi kurudi nyuma sasa. Semina imetoamaelekezo na sualala kuisimamia Serikali lipo palepale,”alisema Sadala.

Kiongozi huyo aliyeteuliwa mwishoni mwa wiki kushika wadhifa huo, alisema CCM kilikuwa kimeanza kuyumba lakini sasa kina matumaini ya kujipanga na kurudi upya.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa Peter Bunyongoli alisema mkakati  waloikbaliana ni  kukirdiisha cama kwa wanacchma  na kupunguza vyeoabavyo baadhi yao walikuwa ni ututiri wa nafasi za kuchagulia.

Bunyongoli alisema kila mmoja alipewa kazi na kueleza mikakati ya namna atakavyifanya atakkaporudi kwenye eneo llake ambbapo wametakiwa kufanya semina kwa watu wa chini yao.

Katibu wa CCM Wilaya ya Korogwe Josephine Mbezi alisema mpango waliofurahishwa nnao ni wa kuwasimamia watendaji ambao tangu awali walona kama chama hakina nguvu kwao.