http://www.swahilihub.com/image/view/-/4928596/medRes/2219971/-/hkfk0z/-/waandamanaji.jpg

 

Maprofesa wa Sudan wampinga Al Bashir

Waandamanaji wanaompinga Rais Omar al Bashir 

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Thursday, January 10  2019 at  08:55

Kwa Muhtasari

Al Bashir amelaani kuchoma mali kwa makusudi na kusababisha madhara.

 

Atabara, Sudan. Mamia ya watu wameandamana Mashariki mwa mji wa Sudan wa Al- Gadarif ikiwa ni katika harakati za kumpinga Rais wa nchi hiyo, Omar al Bashir huku ikidaiwa kuwa maprofesa ndio walioshiriki kuandaa maandamano hayo.

Mashuhuda wanasema kuwa majeshi ya ulinzi yametumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu wanaoandamana kwa wiki ya tatu sasa na ambao walikuwa wakiimbia, ‘Uhuru, Amani na Mapinduzi kwa Sauti ya Wananchi.

Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Maprofesa nchini humo, ambayo inamtaka Rais Bashir kujiuzulu.

Akizungumza katika kituo cha jeshi katika mji wa Atbara, Al Bashir amelaani kile alichokiita usaliti wa kuchoma mali kwa makusudi na kusababisha madhara.

Wakati huohuo Uingereza, Marekani, Canada na Norway zimetoa taarifa ya pamoja, zikisema kwamba zimeshtushwa na taarifa za vifo na kujeruhiwa kwa watu walioshiriki maandamano hayo ya kudai haki zao.

Taarifa hiyo imedai pia kusikitishwa na utumiaji wa silaha za moto unaodaiwa kufanywa dhidi ya waandamanaji.

Katika hatua nyingine maandamano ya kuiunga mkono Serikali ya Al Bashir yanaweza kufanyika leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Maandamano ya kuipinga Serikali kwa mara ya kwanza yalianza katikati ya Desemba mwaka jana kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha. Bei ya mkate ilipanda mara tatu katika baadhi ya maeneo na bei ya mafuta pia ikapanda.