http://www.swahilihub.com/image/view/-/4208960/medRes/1817977/-/14ufbx7z/-/mjaa.jpg

 

Rais Mnangagwa, Mugabe hawapikiki chungu kimoja

Emmerson Mnangagwa

Rais wa Zimbabwe, Bw Emmerson Mnangagwa ahutubia wafuasi wa Zanu-PF awali katika jiji la Harare. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Tuesday, March 13  2018 at  11:03

Kwa Muhtasari

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 94 ameelezea masikitiko yake namna “nilivyong’olewa madarakani” akisema hayuko tayari kukutana na mrithi wake Rais Emmerson Mnangagwa kwa mazungumzo.

 

HARARE, Zimbabwe

RAIS wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 94 ameelezea masikitiko yake namna “nilivyong’olewa madarakani” akisema hayuko tayari kukutana na mrithi wake Rais Emmerson Mnangagwa kwa mazungumzo.

Mugabe alisema hayo wakati mpasuko kati yake na Mnangagwa ukidaiwa “kuongezeka”.

Kwa mujibu wa gazeti la kibinafsi la The Standard, Mugabe amesisitiza kwamba hawezi kujadiliana na Mnangagwa kufikia maridhiano.

Utawala wa miaka 37 wa Mugabe ulifikia kikomo Novemba 15, 2017, baada ya operesheni ya kijeshi ambayo baadhi ya watu waliisifu kama “marekebisho yasiyo ya umwagaji damu”.

Mugabe hivi karibuni aliripotiwa kwamba alikuwa akiunga mkono chama cha National Patriotic Front (NPF) kinachoongozwa na waziri wa zamani Ambrose Mutinhiri.

 

Ripoti ya gazeti

Mutinhiri, mkongwe wa vita vilivyopiganwa miaka ya 70 dhidi ya utawala wa wachache alikutana na Mugabe siku chache tu zilizopita kabla ya kutangaza kwamba   alikuwa ameunda chama kipya.

Gazeti la The Standard mwishoni mwa wiki lilimnukuu Munthihiri akisema haoni uwezekano wa Mugabe na Mnangagwa “kupikika katika chungu kimoja”.