Mwanamitindo azuru Kenya licha ya onyo

Na PAULINE ONGAJI

Imepakiwa - Thursday, April 20  2017 at  16:07

Kwa Mukhtasari

Mwanamitindo Naomi Campbell ameondoa hofu kuhusu usalama nchini Kenya.

 

Hii ni baada ya mwanamitindo huyu mzaliwa wa Uingereza kuzuru humu nchini na hasa katika eneo la Malindi kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Campbell aliwasili nchini siku ya Jumapili ambapo katika mahojiano na wanahabari wa kigeni, mwanamitindo huyu alifichua jinsi alivyoonywa asije nchini Kenya kutokana na sababu za kiusalama.

“Lakini nilisisitiza na kusema kweli nahisi salama. Kuna utulivu hapa na watu hawapaswi kuogopa kuja nchini Kenya,” aliongeza. 

Mbali na kuzuru eneo hilo mwanamitindo huyo alichukua wakati kukaa na watoto ambapo alipigwa picha na kuzichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.