http://www.swahilihub.com/image/view/-/2731054/medRes/1021158/-/3kpk3p/-/283310-01-02.jpg

 

Mwanamume mrefu zaidi India asema wasichana wamemkataa

Dharmendra Singh

Mwanamume wa kimo cha futi 8 inchi 1 anayedai kuwa mrefu zaidi India, Bw Dharmendra Singh, akiwa kibandani Meerut, kilomita 80 kutoka New Delhi Mei 19, 2015. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA NA LEONARD ONYANGO

Imepakiwa - Wednesday, May 27  2015 at  12:35

Kwa Muhtasari

Mwanamume mwenye urefu wa futi nane na inchi moja nchini India Dharmendra Singh, 32, amefichua kuwa ameshindwa kupata mpenzi kutokana na kimo chake.

 

MWANAUME mwenye urefu wa futi nane na inchi moja nchini India amefichua kuwa ameshindwa kupata mpenzi kutokana na kimo chake.

Dharmendra Singh, 32, kutoka eneo la Meerut, Uttar Pradesh, alisema kuwa urefu wake pia umemfanya ajira ambapo sasa amelazimika kutoza ada ya Rupia 10 (Sh15) watu wanaotaka kupiga naye picha. Baadhi hutoroka baada ya kumpiga picha na huwa hawezi kuwakimbiza.

Raia wengi wa India wanamfikia begani Singh na mtu anayeshikilia rekodi ya urefu duniani anamshinda kwa inchi mbili pekee.

“Baadhi ya watu ninaopiga nao picha hukimbia kabla ya kuniliapa,” analalama Bw Singh.

Alisema kuwa wanawake wamekuwa wakimhepa kutokana na urefu wake na hajawahi kupata mpenzi.

'Wanawake hupenda kuzungumza name lakini ninapoonyesha nia ya kutaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao, wanatoweka na kuniacha mpweke,” anaeleza.

'Nilipokuwa chuoni nilikuwa mwoga na sikuweza kutongoza msichana,” anaongezea.

Anasema kuwa kando na kushindwa kupata mpenzi, urefu wake umemletea masaibu tele kwani waajiri wanamkataa.

Sasa Singh amefanya biashara ya picha katika hifadhi ya maonyesho ya vitu vya ajabu ambapo anangojea wateja wa kupiga nao picha ambayo inamwezesha kupata rupia 10,000 (Sh15,000) kwa mwezi.

Singh ambaye amehitimu shahada ya uzamili katika Lugha ya Kihindi, anasema kuwa kimo chake kimemletea masaibu tele.

Anaposafiri ni sharti aandamane na binamu yake, Ravi.

Kuitwa twiga

Familia yake inahisi kuwa Singh alirithi babu yake ambaye alikuwa na urefu wa futi 7.3.

Kulingana na kitabu cha Guiness kinachohifadhi rekodi za dunia, mtu mrefu zaidi duniani ana urefu wa futi 8.3 na anaishi mjini Ankara, Uturuki. Rekodi hiyo iliingizwa katika kitabu hicho mnamo Februari 8, 2011.

Singh anasema kuwa amekuwa akipachikwa majina ya kila aina huku wengi wakimwita ‘twiga’ au ‘ngamia’.

“Baadhi ya watu wanasema kuwa urefu wangu umenifanya kuwa mtu ovyo,” anasema Bw Singh.