http://www.swahilihub.com/image/view/-/4802350/medRes/2138164/-/ifr3yg/-/papa.jpg

 

Papa Francis: Kutoa mimba ni uuaji wa makusudi

Kiongozi wa Kanisa Katoliki dunini, Papa Francis  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Friday, October 12  2018 at  08:48

Kwa Muhtasari

Utoaji mimba ni kosa kubwa kwa sababu halina tofauti na kosa la uuaji

 

Vatican City. Kiongozi wa Kanisa Katoliki dunini, Papa Francis amekilinganisha kitendo cha kutoa mimba kuwa ni sawa na kumwajiri muuaji.

Akingumza na waumini wa Kikristo jana Vatican, Papa Francis alisema kuharibu mimba ni sawa na kumuua mtu.

Kauli hiyo ilikuwa tofauti na waraka uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya mahubiri yake wakati wa ibada ya kuwasalimu waumini kila wiki katika Uwanja wa Mtakafitu Peter.

Alitolea mifano ya vita, unyonyaji na kile alichokiita utamaduni wa uharibifu, pamoja na utoaji wa mimba.

Akizungumzia kuhusu kuharibu mimba za watoto wenye ulemavu, Papa Francis alikosoa ushauri unaotolewa kwa wazazi ambao walitakiwa kuzitoa mimba zao.

Papa alisema watoto wagonjwa ni sawa na mtu mwingine yeyote mwenye uhitaji duniani, kama ilivyo kwa wazee wanaohitaji msaada, au maskini wanaohangaika kujitafutia maisha.

Papa alisema kwamba suala la utoaji mimba ni kosa kubwa kwa sababu halina tofauti na kosa la uuaji ambao watu wanahukumiwa kifo.