http://www.swahilihub.com/image/view/-/4842216/medRes/2164037/-/8hu8e9/-/masisi.jpg

 

Rais Botswana amshambulia Khama

Rais Mokgweetsi Masisi  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Thursday, November 8  2018 at  11:20

Kwa Muhtasari

Ninasikitika kutangaza kwamba juhudi zao hazijazaa matunda 

 

Gaborone, Botswana. Rais Mokgweetsi Masisi ametumia hotuba yake ya kwanza ya taifa kumshambulia waziwazi mtangulizi wake Ian Khama hali inayoibua mgogoro ambao haujawahi kutokea katika taifa ambalo linajisifu kwa utulivu.

Masisi, ambaye alikuwa chaguo la Khama mwenyewe, alichaguliwa kuwa rais Aprili mwaka huu Khama alipong’atuka baada ya kuongoza kwa miaka 10.

Lakini watu wawili hao wamehitilafiana hadharani hali inayotishia kudhoofisha ustawi na sifa ya Botswana iliyojengwa kwa uangalifu hadi kuwa na serikali imara.

“Wananchi wa Batswana wote wanajua kuwa mabadiliko kutoka utawala uliopita hayakuwa shwari kama ilivyotarajiwa,” Masisi alisema alipolihutubia taifa Jumatatu akitumia neno kwa watu wa Botswana.

Alisema alijaribu “kurahisisha mchakato” kwa kuteua wanasiasa waandamizi kujadiliana na Khama.

“Ninasikitika kutangaza kwamba juhudi zao hazijazaa matunda,” Masisi alisema, akiongeza kuwa sababu kubwa ya msuguano ilikuwa haki za kustaafu na pensheni anazopaswa kupata Khama.

Khama inadaiwa amekasirishwa na hatua ya Masisi kukataa kumruhusu kutumia ndege za Serikali.