http://www.swahilihub.com/image/view/-/4369558/medRes/1927556/-/12v66ab/-/tshisekedi.jpg

 

Rais Tshisekedi augua ghafla akitoa hotuba

Mwanawe Tshisekedi ateuliwa kuwania urais DRC

Felix Tshisekedi. Picha/MAKTABA 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Friday, January 25  2019 at  14:27

Kwa Muhtasari

Rais Felix Tshisekedi ameahidi kusimamia suala la demokrasia na amani DRC.

 

KINSHASA, DRC

RAIS mpya wa Jamhuri ya Kidemokarsia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi ameugua ghafla wakati akitoa hotuba muda mfupi baada ya kuapishwa jana Alhamisi.

Rais Tshisekedi mara baada ya kula kiapo alitoa hotuba kwa wananchi waliokuwa wamehudhuria sherehe hiyo lakini alishindwa kuendelea na kusema kwamba anajisikia vibaya hawezi kuendelea kuongea.

“Sijisikii vizuri,sijisikii vizuri kabisa ‘‘alisema rais huyo na kuacha kuendelea kuhutubia taifa

Awali akitoa hotuba yake alisema atahakikisha anasimamia demokrasia na amani nchini humo ambayo imepotea kwa muda mrefu.

Alisema atahakikisha amani iliyotoweka inarudi kama zilivyo nchi nyingine za Afrika na pia aliwaomba wanasiasa wote waliokuwa kwenye kinyang’anyiro cha urais kutoa ushirikiano ili kuhakikisha nchi inakuwa na amani.

Alisema atalinda rasilimali za nchi ili kukuza uchumi na kutekeleza ahadi ambazo alizitoa wakati wa kampeni zake za kuwania urais.

Pia aliwaomba wagombea hao kukubali kushindwa akidai hakuna ushindani usiokuwa na mshindi na kukubali kushindwa ni sehemu ya demokrasia.

Aliwataka wapinzani wake wasahau tofauti zote na badala yake washirikiane kuijenga DRC.

 

Haki

Alisema ana hakika Mahakama ya Katiba ilitenda haki kutoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mpinzani wake Martin Fayulu.

Tukio la kuapishwa lilifanyika mjini Kinshasa mchana jana na kuhitimisha utawala wa karibu miongo miwili ya Rais anayeondoka madarakani, Joseph Kabila.

Katika hotuba yake ya kwanza tangu uchaguzi, Kabila alihimiza Umoja wa Kitaifa na kusema kuwa anatoa wito huo kwa muungano mkuu wa wadau wote wanaopenda maendeleo.

Kabila alijitapa kwa kufanikisha mengi ikiwa ni pamoja na kuliunganisha taifa na kudhibiti mfumuko wa bei.