http://www.swahilihub.com/image/view/-/4925626/medRes/2218069/-/bwlj10/-/mapangou.jpg

 

Serikali Gabon yadai kuzima jaribio la mapinduzi

Waziri wa Mawasiliano wa Gabon, Guy-Bertrand Mapangou 

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Tuesday, January 8  2019 at  09:57

Kwa Muhtasari

Wanajeshi waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa

 


 

Gabon. Serikali ya Gabon imedai kwamba imefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi nchini humo dhidi ya Rais Ali Bongo ambaye anapatiwa matibabu nchini Morocco.

Waziri wa Mawasiliano wa Gabon, Guy-Bertrand Mapangou aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwamba wanajeshi waaminifu kwa Serikali ya Rais Bongo wamefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya Serikali nchini humo.

Mapangou alisema wanajeshi wanne waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa na mwingine wa tano anasakwa.

“Hali ni tulivu. Polisi ambao huwa hapo wamerejea na kuchukua udhibiti wa eneo lote la makao makuu ya mashirika ya redio na runinga, kwa hivyo kila kitu kimerejea kawaida,” alisema.

Mapema jana asubuhi, kundi la wanajeshi lilitangaza kutekeleza mapinduzi ya Serikali katika Taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje.