Trump aamuru muuaji wa watu wanne New York anyongwe

Na AFP

Imepakiwa - Thursday, December 7  2017 at  18:23

Kwa Muhtasari

Rais Donald Trump aliamuru Jumatano kwamba mwanamume mmoja aliyewaua watu wanane jijini New York kwa kuwagonga kwa gari, kimakusudi, ahukumiwe kifo.

 

RAIS Donald Trump aliamuru Jumatano kwamba mwanamume mmoja aliyewaua watu wanane jijini New York kwa kuwagonga kwa gari, kimakusudi, ahukumiwe kifo.

“Gaidi huyo alifurahi pale alipoomba kuwa bendera ya kundi la ISIS iwekwe kwenye chumba chake hospitalini. Aliwaua watu wanane na kuwajeruhi wengine 12. Anafaa kupewa hukumu ya kifo!” Trump akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, akirejelea kundi la Islamic State.

Mapema rais huyo alikuwa anawaza kuamuru mshukiwa huyo kwa, Sayfullo Saipov, apelekwe Guantanamo Bay nchini Cuba ambako magaidi wa kigeni kuzuiliwa.

Mtindo huo wa kuwazuia washukiwa wa kigaidi katika kambi hiyo ya kijeshi, umekosolewa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu.

Jumatano wachunguzi walisema mwanamume huyo alikiri kuwa alitenda mauaji hayo “kwa jina la ISIS” na kwamba alifurahia kwa mauaji hayo.

Waendesha mashtaka wamemfungulia mashtaka mshukiwa huyo wa umri wa miaka 29 ambaye ni mhamiaji ambaye ni Uzbekistan. Walisema jamaa huyo amekuwa akipanga shambulio hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Saipov alishtakiwa kwa makosa mawili ya: kutoa usaidini kwa kundi moja la kigaidi na uharibifu wa magari kadhaa.
Rais wa Uzbekistan alisema serikali yake imejitolea kusaidia Amerika kuchunguza kisa tukio hilo.