http://www.swahilihub.com/image/view/-/3785954/medRes/1483762/-/k309cm/-/dasa.jpg

 

Trump achunguzwa kubaini ikiwa alijaribu kuzima uchunguzi

Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Friday, June 16  2017 at  13:38

Kwa Mukhtasari

Misukosuko imeendelea kumsakama Rais Donald Trump baada ya kuanza kuchunguzwa dhidi ya tuhuma kwamba alizuia uchunguzi kuhusu uwezekano wa Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani uliofanyika Novemba 2016.

 

WASHINGTON, Marekani

MISUKOSUKO imeendelea kumsakama Rais Donald Trump baada ya kuanza kuchunguzwa dhidi ya tuhuma kwamba alizuia uchunguzi kuhusu uwezekano wa Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani uliofanyika Novemba 2016.

Taarifa ya kuchunuzwa kwa Rais Trump imekuja siku chache baada ya wabunge takriban 200 wa Chama cha Democratic kumfungulia kesi kiongozi huyo inayohusu mgongano wa kimaslahi inayotokana na himaya ya biashara zake kupokea fedha kutoka taasisi za kigeni.

Juzi, Gazeti la Washington Post la Marekani lilimnukuu Mkuu wa Tume Maalumu ya kuchunguza madai  ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani Robert Mueller akisema anachunguza uwezekano wa Rais Trump kuingilia uchunguzi huo. Taarifa ya gazeti hilo ilieleza kwamba maofisa waandamizi wa upelelezi katika Serikali wamekubali kuhojiwa na wachunguzi wa Tume maalumu ya Robert Mueller. 

Maofisa waliokubali kuhojiwa wiki hii ni Daniel Coats ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi, Admiral Mike  Rogers ambaye ni Mkuu wa Shirika la Usalama wa Taifa (NASA) na Richard  Legett naibu wake aliyeacha  kazi hivi karibuni.

Taarifa ya gazeti hilo ilipokewa kwa hasira  na timu ya mawakili wa Rais Trump na msemaji wake Mark  Corallo akisema uvujishaji huo wa taarifa  kumhusu Trump na wafanyakazi wa FBI unachukiza, hausameheki na ni kinyume cha sheria.

Gazeti hilo lilisema uamuzi wa kuchunguza madai ya kuingilia uchunguzi huo ulianza siku kadhaa baada ya Rais Trump kumfuta kazi Mkurugenzi wa FBI James Comey, Mei 9, 2017.

Mueller anaongoza uchunguzi wa FBI kuhusu Urusi  kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na kuwapo kwa uhusianao wowote wa Trumo katika suala hilo. Hata hivyo  Rais Trump amekana mara  kadhaa kuhusika katika suala hilo.

Kufukuzwa kazi kwa Comey kunaelezwa kulitokana na

jitihada za Rais Trump kumshawishi mkurugenzi huyo aachane na  uchunguzi dhidi ya mshauri wake wa masuala ya usalama  Michael  Finn.

Finn alifukuzwa kazi mwezi Februari kwa kushindwa kufichua kiwango cha uhusiano wake na Sergei Kislyak ambaye ni balozi wa Urusi nchini Marekani.

Vitengo vya kijasusi nchini Marekani vinaamini kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani ili kumsaidia Donald Trump.

 

Ushahidi wa Comey wamuweka kitanzini

Wataalamu wa masuala ya sheria wamesema kuwa ushahidi wa Comey wiki iliyopita kwamba Trump  alitarajia utiifu kutoka kwake na kwamba aliamini angeacha na uchunguzi dhidi ya Flynn na hivyo kusaidia kuepuka madai ya uingiliaji wa uchunguzi huo.

Kosa la kuzuia utekelezaji wa haki linaweza kujenga msingi wa kuanzisha mchakato wa kuondolewa madarakani kwa Trump.