http://www.swahilihub.com/image/view/-/4800874/medRes/2137230/-/vn4s9iz/-/trump.jpg

 

Trump akubali kujiuzulu kwa Balozi UN, amtaka kuwania nafasi nyingine

Rais Donald Trump akiwa na Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa (UN), Nikki Haley  

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Thursday, October 11  2018 at  09:25

Kwa Muhtasari

Natumaini utapenda kurudi wakati fulani baadaye lakini katika majukumu mengine

 

Washington, Marekani. Rais Donald Trump amekubali kujiuzulu kwa Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley, akisema ataachia majukumu yake mwishoni mwa mwaka.

Akiwa Ikulu Jumanne, Trump alimtaja balozi Nikki kuwa “mtu maalum sana” ambaye anafanikisha,” akiongeza kuwa alimwambia miezi sita iliyopita kuwa alihitaji muda wa kupumzika.

Haley, mwenye umri wa miaka 46, alisema hakuwa na mipango ya haraka, na alikanusha kuwa atawania urais mwaka 2020.

Trump alisema Jumanne kuwa anaweza “kumchukua” tena kumpa kazi ikiwa atahitaji kurudi kwenye utawala.

“Sisi sote tunakufurahia kwa njia moja, lakini tunachukia kushindwa - natumaini utapenda kurudi wakati fulani baadaye lakini katika majukumu mengine tofauti. Unaweza kuchagua,” alisema. (CNN).