http://www.swahilihub.com/image/view/-/1348942/medRes/1181938/-/p8d2uyz/-/dn2firstzimbabwe3.jpg

 

Walinzi wa mke wa Mugabe waondolewa

mugabe

Grace Mugabe, mkewe Robert Mugabe wa Zimbabwe. Picha/AFP 

Na AFP

Imepakiwa - Thursday, January 11  2018 at  22:12

Kwa Muhtasari

SERIKALI ya Zimbabwe imeondoa walinzi wa aliyekuwa Mama Taifa Grace Mugabe huku wengi wa wasaidizi wake walipewa majukumu mengine, duru zimesema.

 

Walinzi hao wataondolewa “hatua kwa hatua hadi Jumatatu wiki ujao.” kulingana na afisa wakuu serikali waliohojiwa na shirika la habari la NewsDay.

Bi Mugabe alikuwa ametengewa maafisa wa ulinzi kabla ya kuondolewa kutokana chama tawala cha Zanu- PF ambapo alikuwa akishikilia wadhifa wa kiongozi wa kundi la wanawake wanachama wa chama hicho.

“Walinzi wake wanaendelea kuondolewa hatua kwa hatua,” afisa huyo ambaye hakutaka kutajwa alinukuliwa akisema.
Baadaye Grace atakuwa akitegemea kikosi cha walinzi kilichotengewa Rais wa zamani Robert Mugabe. Sasa hatakuwa usemi katika utendakazi wa walinzi hao sababu hawatakuwa wakiwajibika, moja kwa moja, kwake.

Hata hivyo, msemaji wa serikali George Charamba hakuthibitisha habari hizo lakini akasema: “Kimsingi, naamini serikali haitamudu kugharamia usalama wa Chatunga (kitinda mimba wa Mzee Mugabe) anapotaka kusafiri hadi Amerika au akiamua kuishi kule. Familia hiyo itakuwa ikitegemea walinzi wa Rais wa zamani.

Haya yanajiri wiki chacha baada ya Rais wa Zimbabwe Emmernson Mnangangwa kuahidi kuwa atamtunza Mzee Mugabe, 93, katika uhai wake.

Serikali ya Zimbabwe juzi ilichapishwa kanuni zinazoelezea manufaa ambayo marais wa zamani wanapaswa kupewa wakiwa nje ya afisi.

Baadhi ya manufaa hayo ni kama vile walinzi, wapishi, wafanyakazi wa nyumbani, nyumbani mbili, msafara wa magari na ziara nne za kimataifa kila mwaka. Manufaa hayo yote yatagharamiwa kwa pesa za walipa ushuru.

Wiki iliyopita Mzee Mugabe alisafiri ng’ambo kwa shughuli za kimatibabu.