WhatsApp kuwezesha watumiaji kufuta ujumbe waliotuma

WhatsApp

Nembo ya mtandao wa kijamii wa simu WhatsApp. Picha/HISANI 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Wednesday, January 11  2017 at  14:26

Kwa Mukhtasari

MTANDAO maarufu wa kijamii WhatsApp upo kwenye pilka pilka za kuwawezesha watumiaji wake kufuta ujumbe waliokwishwa utuma pasi na kupokelewa na upande wa pili.

 

Kuna kipindi unaweza ukawa umetuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika WhatsApp na ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshatumwa na kupokelewa.

Lakini kwa sasa WhatsApp imekuja na wazo la kurekebisha tukio kama hilo kwenye simu za iOS ambapo kutakuwepo na kituge katika eneo la ‘Settings’ kisha ‘Edit’ halafu ‘Revoke’ litakalokuwa likikuwezesha kufuta ujumbe huo kwa wakati mara tu unapogundua ni kosa.

Hata hivyo kikubwa ni kwamba utaweza kufanya hivyo kama tu mtumiaji mwingine bado hajausoma ujumbe huo na kama akishausoma basi hutaweza kuufuta.

Lakini hadi sasa WhatsApp hawajatoa taarifa rasmi ya lini uwezo huo utaanza kutumika.