Zambia yawafukuza raia 30 wa China

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Friday, June 16  2017 at  13:49

Kwa Mukhtasari

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema kuwa raia wake waliokuwa wakishikiliwa nchini Zambia kwa tuhuma za uchimbaji haramu wa madini wameachiwa na wako njiani kuelekea kwao.

 

LUSAKA, Zambia

WIZARA ya Mambo ya Nje ya China imesema kuwa raia wake waliokuwa wakishikiliwa nchini Zambia kwa tuhuma za uchimbaji haramu wa madini wameachiwa na wako njiani kuelekea kwao.

China ilikuwa imeilalamikia Zambia ikisema hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Wachina hao 31 miongoni mwao akiwamo mwanamke mjamzito.

Hata hivyo, Idara ya Uhamiaji ya Zambia imesisitiza kuwa Wachina hao watafukuzwa nchini Zambia.

China imewekeza kiasi cha dola bilioni moja katika sekta ya madini nchini Zambia lakini Wachna wanachukiwa kwa kuhuma za kuwanyanyasa na kuwalipa wenyeji mishahara duni.

Mwaka 2012 wafanyakazi walimuua msimamizi wao wa Kichina na kumjeruhi vibaya mwingine katika mzozo wa wa malipo kwenye mgodi wa makaa ya mawe.

Mwaka mmoja kabla, polisi nchini humo iliwahukumu wasimamizi wa Kichina kwa jaribio la kuua baada ya Wachina kufyatua risasi katika mzozo mwingine wa malipo.