http://www.swahilihub.com/image/view/-/4924122/medRes/2217121/-/1ptmupz/-/zuma.jpg

 

Zuma na safari ya muziki

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma 

Na Mwandishi Wetu

Imepakiwa - Monday, January 7  2019 at  09:11

Kwa Muhtasari

Alikuwa wa kwanza kuimba nyimbo za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.


 

Durban, Afrika Kusini. Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ametangaza kuanza kwa kazi yake mpya katika muziki. Kazi hii itaanza Aprili kwa nyimbo za kupigania uhuru wa Afrika Kusini.

Zuma, mwenye umri wa miaka 76 alisaini mkataba na manispaa ya Durban, ambayo ilikubali kufadhili albamu ya nyimbo za kupigania uhuru zilizoimbwa na Zuma. Chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimesema mkataba huo una shaka ndani yake.

Zuma aliimba nyimbo nyingi za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi wakati wa kazi yake ya kisiasa.

Katika kila mkutano wa ANC, mara nyingi alikuwa wa kwanza kuinuka, na kuanza kuimba nyimbo za mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Nyimbo hizo ndizo zimemfanya kuwa maarufu nchini Afrika Kusini.