http://www.swahilihub.com/image/view/-/2908984/medRes/876339/-/rxi7mrz/-/415642-01-02%25282%2529.jpg

 

Afisa serikalini Korea Kaskazini auawa kwa kukaa vibaya

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un akihudhuria mkutano wa wakuu wa jeshi la nchi hiyo awali. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Wednesday, August 31  2016 at  08:02

Kwa Muhtasari

Naibu Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Korea Kaskazini ameuawa kwa kutumia bunduki za kuangusha ndege kwa kile uongozi unadai ni kukosa heshima kwenye mkutano ulioongozwa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-Un.

 

SEUOL, Korea Kusini

NAIBU Kiongozi wa ngazi ya juu nchini Korea Kaskazini ameuawa kwa kutumia bunduki za kuangusha ndege kwa kile uongozi unadai ni kukosa heshima kwenye mkutano ulioongozwa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-Un.

Maafisa wengine wawili wenye makosa kama hayo nao wametimuliwa nchini humo, kwa mujibu wa taarifa kutoka Korea Kusini.

Tangu achukue hatamu za uongozi wa Korea Kaskazini tangu kifo cha babake 2011, inaaminika Kim ameua au kutimua viongozi wenye nyadhifa kuu serikalini katika kile wachanganuzi wanasema ni kuufanya uongozi wake uwe dhabiti zaidi.

"Naibu Kiongozi wa elimu Kim Yong-Jin ameuawa," Wizara ya Utangamano ya Korea Kusini kupitia kwa msemaji wake Jeong Joon-Hee imesema kwenye kikao na wanahabari.

Taarifa zinasema Kim Yong-Jin aliuawa kwa kukaa vibaya kwenye jukwaa moja na Kim Jong-Un japo afisa aliyezitoa amedinda kutajwa.