http://www.swahilihub.com/image/view/-/4369558/medRes/1927556/-/12v66ab/-/tshisekedi.jpg

 

Rais Magufuli ampongeza Tshisekedi kuwa Rais wa DRC

Mwanawe Tshisekedi ateuliwa kuwania urais DRC

Felix Tshisekedi. Picha/MAKTABA 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Monday, January 21  2019 at  09:30

Kwa Muhtasari

Rais John Magufuli amempongeza kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi kwa kuibuka mshindi katika mbio za urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

DAR/KINSHASA

RAIS John Magufuli amempongeza kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi kwa kuibuka mshindi katika mbio za urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Salamu hizo zimekuja siku moja baada ya Mahakama ya Katiba ya Congo kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa na kiongozi mwingine wa Muungano wa Vyama vya Upinzani (UPC) aliyetaka matokeo ya awali yatenguliwe na kura kuhesabiwa upya.

Katika salamu zake alizotoa kwa kutumia akaunti yake ya Twitter, Rais Magufuli amemtaka mteule huyo kusimamia amani na kumuahidi kwamba uhusiano wa karibu wa Tanzania na Congo utaendelea.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa alithibitisha kuwa ujumbe uliotumwa katika akaunti hiyo ya Twitter jana wa kumpongeza Tshisekedi ni wa Rais Magufuli.

Jijini Kinshasa, Mahakama ya Kikatiba ya Congo imemthibitisha Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Desemba 30, 2018.

Mahakama hiyo ilitupilia mbali madai ya kiongozi wa upinzani Martin Fayulu kwamba uchaguzi huo ulikuwa na udanganyifu.

Fayulu anadai kwamba Tshisekedi na Joseph Kabila walifanya mpango wa siri na baada ya matokeo ya awali kuonyesha kuwa Emmanuel Shadary, mgombea ambaye alikuwa akiungwa mkono na Kabila, ameshika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo.