http://www.swahilihub.com/image/view/-/4748184/medRes/2102450/-/11tq1xpz/-/albert.jpg

 

Barua inayokana uwepo wa Mungu yauzwa kwa Sh290 milioni

Albert Einstein

Picha ya mwanasayansi Albert Einstein (1879-1955) katika Taasisi ya Teknolojia ya California (Caltech), 1931. Picha/KABRASHA LA HISTORIA 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Wednesday, December 5  2018 at  14:59

Kwa Muhtasari

Barua ya mwanasayansi wa Ujerumani Albert Einstein iliyoandikwa kwa hati ya mkono zaidi ya miaka 50 iliyopita, ikikana uwepo wa Mungu imeuzwa kwa Sh289 milioni.

 

NEW YORK, Marekani

BARUA ya mwanasayansi wa Ujerumani Albert Einstein iliyoandikwa zaidi ya miaka 50 iliyopita, ikikana uwepo wa Mungu imeuzwa kwa Sh289 milioni.

Barua hiyo iliyoandikwa kwa hati ya mkono ilipigwa mnada Jumanne na kupitisha Sh150 milioni zilizokadiriwa kuwa thamani ya barua hiyo.

Hii ni mara tatu kwa barua hiyo kupigwa mnada.

Mnamo 2002, barua ilipigwa mnada na kuuzwa kwa Sh210 milioni.

Katika barua yake aliyoandika mnamo 1954, mwanafizikia Einstein, alimweleza mwanafilosofia Eric Gutkind kuwa, hakuamini kuwepo kwa Mungu.

"Kwangu, neno Mungu halina maana yoyote. Jina hilo linatokana na unyonge wa binadamu," akasema Einstein.

Mwanafizikia huyo aliyeaga dunia mnamo 1955, alisema kuwa Biblia ni kitabu cha hekaya za abunuwasi.

Barua hiyo ilipigwa mnada kwa mara ya mwisho mnamo  2008 kwa Sh40 milioni.