http://www.swahilihub.com/image/view/-/4918642/medRes/2213507/-/juuy9kz/-/mtambo.jpg

 

Data zinazodaiwa kufuja zaonyesha nani kashinda urais DRC

CENI

Mfanyakazi wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) aukagua mtambo wa kupigia kura Desemba 20, 2018. Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Wednesday, January 16  2019 at  14:46

Kwa Muhtasari

Mahakama ya Katiba DRC tayari imeanza kesi ya uchaguzi.

 

KINSHASA, DRC

MAHAKAMA ya Kikatiba katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza kusikiliza ombi la kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyompa ushindi kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi, lililowasilishwa na mpinzani mwingine, Martin Fayulu.

Fayulu alisema matokeo hayo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Felix Tshsekedi kuwa ni “yamepinduliwa”.

Tayari data zinazodaiwa kufuja kutoka kwa Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, Ceni, na ambazo mashirika kama Financial Times la Uingereza na Redio RFI ya Ufaransa, zinaonyesha mshindi alikuwa ni Fayulu wa muungano wa Lamuka.

Zinasema alipata ushindi kwa kujizolea asilimia 59.4 ya kura.

Hata hivyo Ceni ilipotafutwa na FT kujibu tuhuma hizo ilisema matokeo yake hayajachakachuliwa.

Matokeo ya awali ya uchaguzi yamempatia Tshisekedi asili mia 38.57 ya kura dhidi ya asili mia 34.8 za Fayulu.

Mgombea anaeungwa mkono na rais Joseph Kabila Emmanuel Ramazani Shadary amemaliza wa tatu kwa kujikingia asili mia 23.8.

Martin Fayulu anabisha matokeo hayo na kusema ameshinda kwa asili mia 61 ya kura. Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ataapishwa Januari 22 inayokuja.