Jaribio la mapinduzi 2016 lawaponza kazi Waturuki 7,000

Jaribio la mapinduzi Uturuki

Afisa wa Polisi wa Uturuki (kulia) amkumbatia mwanamume katika kifaru eneo la Uskudar, Istanbul baada ya polisi kuchukua nafasi ya wanajeshi waasi waliojaribu kuipindua serikali ya taifa hilo Julai 16, 2016. Picha/AFP 

Na SAMMY WAWERU na MASHIRIKA

Imepakiwa - Saturday, July 15  2017 at  17:58

Kwa Mukhtasari

Maafisa 7,000 wa Uturuki yumkini wanajutia 'kuhusika' katika jaribio la kupindua serikali ya nchi hiyo baada yao kupigwa kalamu.

 

MAAFISA 7,000 wa Uturuki yumkini wanajutia 'kuhusika' katika jaribio la kupindua serikali ya nchi hiyo baada yao kupigwa kalamu.

Maafisa hao ni polisi, maafisa wa serikali na wasomi wanaohusishwa na jaribio la mapinduzi ya serikali mwaka 2016.

Ni uamuzi umetekelezwa Jumamosi Julai 15 wakati wa kuadhimisha mwaka wa kwanza tangu jaribiio hilo kufanyika.

Duru zaarifu zaidi ya watu 250 waliuawa kabla ya jaribio hilo kuzimwa na wanajeshi walioa waaminifu kwa Serikali.

Imesemekana hatua hiyo ni moja wapo ya kuwaondoa watu wasio waaminifu ambapo kufikia sasa zaidi ya watu 200,000 wameachishwa kazi.

"Wao ndio walijichimbia kaburi lao kwa kuunga mkono wapangaji wa mapinduzi hayo yaliyopangwa na kiongozi wa kidini aliye uhamishoni Marekani, Fethullah Gulen," akasema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Kwingineko, mke wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Grace Mugabe ameripotiwa kupata majeraha madogo katika ajali ya barabara lakini Rais Mugabe hakuumia popote.

Vyombo vya habari vya serikali vinasema ajali hiyo ilitokea wakati familia hiyo ilikuwa ikitoka uwanja wa ndege wa Harare.

Vimeongeza kuwa walikuwa wamerudi kutoka Singapore ambapo Rais Mugabe alikuwa ameenda kupokea matibabu.

"Grace alipata jeraha katika mkono wake kwenye ajali ndogo ya barabarani iliyohusisha msafara wa Rais," vikaarifu vyombo vya habari Zimbabwe.

Aidha alitibiwa katika kliniki moja na kuruhusiwa kwenda nyumbani bila majeraha makubwa. 

"Mke wa rais alilalamikia uchungu katika mkono wake lakini hakuelezea kiini cha ajali hiyo," Msemaji wa serikali nchini humo akaeleza waandishi wa habari Jumamosi mjini Harare.

Hata hivyo shahidi mmoja alidokeza kuwa aliona mwili uliotengwa wa mwendeshaji pikipiki wa msafara wa Rais Mugabe katika eneo hilo.

Visa kadhaa vya ajali vinavyohusisha msafara huo wa Rais vimekuwa vikishuhudiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Msafara huo una magari 10 yenye ving'ora vya kuyaonya magari mengine.

Rais Mugabe alizaliwa Februari 21, 1924 na amekuwa usukani kama rais tangu mwaka wa 1980.