http://www.swahilihub.com/image/view/-/3483922/medRes/1510940/-/h9d5psz/-/dangota.jpg

 

Serikali yatakiwa kuchukua ushauri wa Aliko Dangote

Aliko Dangote

Bwanyenye raia wa Nigeria, Aliko Dangote akihutubia wanahabari mnamo 2014. Picha/AFP 

Na IBRAHIM YAMOLA

Imepakiwa - Thursday, October 12  2017 at  07:52

Kwa Mukhtasari

Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) ilisema Tanzania inapaswa kuufanyia kazi na si kuupuuza ushauri uliotolewa na bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote.

 

DAR ES SALAAM, Tanzania

TAASISI ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) ilisema Tanzania inapaswa kuufanyia kazi na si kuupuuza ushauri uliotolewa na bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote.

Juzi Dagote alimtahadharisha Rais John Magufuli kuwa vitendo vyake vinaogofya na kuwakimbiza wawekezaji nchini.

Dangote alilaumu sera za Serikali akisema.” Sera zake zinawakatisha tamaa wawekezaji wengi na si kitu kizuri. Mmoja zinawakatisha tamaa na wengine watakimbia hata bila kuhitaji maelezo.

Malalamiko hayo aliyatoa jiini London, Uingereza alikohutubia kongamano la wawekezaji wa Afrika lililoandaliwa na gazeti la Finanial Times.

Akitoa maoni yake Jumanne kuhusu kauli hiyo ya Dangote, Mkurugenzi Mkuu wa TPSF Godfrey Simbeye alisema mwekezaji huyo ni mkubwa na anapozungumza anasikika ndani na nje ya Afrika hivyo kutofanyia kazi ushauri wake kunawea kuligharimu Taifa. Alichokisema ni ushaui na Dangote ni mwekezaji mkubwa amewekeza ndani na nje ya Afrika. Sidhani kama ushauri wake unaweza usifanyie kazi na mimi nashaui ufanyiwe kazi na si kuupuuza,” alisema Simbeye na kuongeza,” Serikali iufanyie kazi kama ana hoja zifanyiwe kazi si kuzipuuza na kama hana hoja ajibiwe. Yule si mtu wa kubeza. Mtu kama huyo ni mwekezaji mkubwa na anapozungumza kitu tunapaswa kukiona na kukifanyia kazi. Ni wakati Serikali kupokea ushauri wake.

Simbeye alisema kwa uzoefu wake katika nchi mbalimbali anachokizungumza mfanyabiashara huyo kina tija hivyo  ni wakati sasa Serikali kupokea ushauri huo.

Kwa upande wake, kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe alisema Serikali isikilize na kuufanyia kazi ushauri wa Dangote kwani kwa kawaida mitaji huona aibu.

Serikali ijiondoe kwenye dhana kwamba uwekezaji ni kupata kodi tu, la hasha,” alisema mbunge huyo wa Kigoma mjini.

Aliongeza, “Kwa demografia ya Tanzania ambapo watu 1.6 milioni huingia kwenye soko la ajira kwa mwaka, ajira yapaswa kuwa lengo kubwa la Serikali katika kuvutia mitaji kutoka nje na vilevile ndani ya nchi.

Kuimarisha uwekezaji

Mtaalamu wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Humphrey Moshi alisema ufike wakati wawekezaji wasigeuke miungu kwa watu wadogo huku akiishauri Serikali kuendelea na mikakati yake ya kuimarisha uwekezaji.

“Tumpuuze tu, mazingira ya sasa ya biashara yanahitaji uwazi. Ili uwe wazi lazima upinge rushwa na dhana ya ‘win-win situation’. Unapomwona mwekezaji kaja kwako kuna kitu kakiona. Sasa ukiona anaanza kusema vikwazo, kuna jambo,” alisema Profesa Moshi.

Hata hivyo, akizugumza na Mwanachi jana, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage alisema, “Mimi sina ubishi na Dangote na hatuwezi kupuuza ushauri wake kwani uwapo kwake hapa nchini kumewezesha kufanikisha kubadili hata bei ya saruji.”

“Nimeshazungumza na Dangote na amekwisha kuzungumza pia na viongozi wangu wa juu na tunatambua uwekezaji wa Dangote hapa nchini”, alisisitiza Mwijage.

Malalamiko ya Dangote yanatokana na sheria mpya ya usimamizi wa rasilimali za Taifa iliyopitisha na Bunge mwezi Juni inayopendekeza Serikali kuwa na walau asilimia 16 kwenye miradi yote ikiyowekezwa kwenye sekta ya Madini.