http://www.swahilihub.com/image/view/-/2523138/medRes/876339/-/n7scbb/-/415642-01-02%25282%2529.jpg

 

Korea Kaskazini yatishia kufuta mkutano uliopangwa wa Kim Jong Un na Trump

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un akihudhuria mkutano wa wakuu wa jeshi la nchi hiyo mapema Novemba, 2014. Picha/AFP 

Na AFP

Imepakiwa - Wednesday, May 16  2018 at  14:06

Kwa Muhtasari

Serikali ya Korea Kaskazini imetishia kufutilia mbali mkutano kati ya kiongozi wake, Kim Jong Un na Rais Donald Trump kama nchini Marekani itawalazimisha kusalimisha silaha za nyuklia.

 

PYONGYANG, Korea Kaskazini

SERIKALI ya Korea Kaskazini imetishia kufutilia mbali mkutano kati ya kiongozi wake, Kim Jong Un na Rais Donald Trump kama nchini Marekani itawalazimisha kusalimisha silaha za nyuklia.

Serikali hiyo pia ilifutilia mbali mkutano uliotarajiwa kufanyika jana kati ya maafisa wa kuu wa nchi hiyo na wa Korea Kusini.

“Kama Marekani inajaribu kutubana na kutulazimisha kusalimisha silaha zetu, hatutakuwa tena na hitaji la mashauriano,” naibu waziri wa mambo ya kigeni Kim Kye Gwan, amesema kwenye taarifa iliyopeperushwa na shirika la habari la taifa.

Kutokana na hali hiyo, aliongeza kuwa imebidi Korea Kaskazini ifikirie upya kama itashiriki katika mkutano uliopangiwa kufanyika Singapore mnamo Juni 12.

Ilikuwa imepangwa kuwa silaha za nchi hiyo iwe ni ajenda kuu itakayojadiliwa katika mkutano huo uliotarajiwa kuwa wa kihistoria, ingawa Korea Kaskazini imekuwa ikisisitiza inahitaji silaha hizo kwa ulinzi wake dhidi ya shambulio linaloweza kufanywa na Marekani.

Marekani inataka thibitisho kamili kwamba Korea Kaskazini haitakuwa na silaha za kinyuklia na itaendelea kupanga mkutano huo.