http://www.swahilihub.com/image/view/-/2868740/medRes/1118121/-/271ijjz/-/742150-01-02%25282%2529.jpg

 

Mfalme wa Saudi Arabia kushauriana na Putin jijini Moscow

Mfalme Salman bin Abdulaziz

Mfalme Salman bin Abdulaziz (kulia) wa Saudi Arabia ampa matumaini na kumtuliza manusura wa mkasa wa kreni katika hospitali ya msikiti mkuu wa Mecca Septemba 12, 2015. Picha/AFP 

Na SAMMY WAWERU na MASHIRIKA

Imepakiwa - Thursday, October 5  2017 at  08:28

Kwa Muhtasari

Mfalme wa Saudi Arabia Salman Jumatano jioni aliwasili jijini Moscow, Urusi ili kujadiliana namna mataifa hayo mawili yanaweza 'kuishi vizuri'.

 

MOSCOW, Urusi

MFALME wa Saudi Arabia Salman Jumatano jioni aliwasili jijini Moscow, Urusi ili kujadiliana namna mataifa hayo mawili yanaweza 'kuishi vizuri'.

Ziara hiyo ndiyo ya kwanza Urusi kwa Mfalme Salman tangu aingie mamlakani.

"Kwenye ziara yake atafanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladmir Putin. Hiyo ni njia moja ya kuimarisha uhusiano wao wa karibu katika siku za karibuni," imeripoti CNN mapema Alhamisi.

Mataifa hayo mawili yanatambulika duniani katika uzalishaji na usafirishaji wa mafuta.

Aidha majadiliano kati ya viongozi hao yanatarajiwa kulenga ushirikiano wa uzalishaji wa mafuta pamoja na kutia sahihi mikataba kadhaa ya uwekezaji.

"Swala la Syria, nchi ambayo Saudia Arabia na Urusi zimekuwa zikiunga mkono katika vita vinavyoendelea pia utazungumziwa," imeeleza CNN.

Katika siku za hivi karibuni, Urusi imekuwa ikishutumiwa kuingilia uchaguzi wa Marekani ambapo inakisiwa kumsaidia Rais Donald Trump kuibuka mshindi.

Serikali ya Marekani kwa sasa inaendelea kuchunguzwa kutokana na madai hayo.