http://www.swahilihub.com/image/view/-/4302804/medRes/1883713/-/vy628dz/-/renamo.jpg

 

Rais Nyusi atangaza mpango mahususi na Dhlakama

Filipe Nyusi

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ahutubia taifa Februari 7, 2018, katika makazi yake jijini Maputo kuelezea mazungumzo ya amani na Vuguvugu la Pingamizi Msumbiji (Renamo). Picha/AFP 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Tuesday, February 13  2018 at  11:41

Kwa Mukhtasari

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji wiki iliyopita alitangaza mpango wa ugawanaji madaraka na Rais wa Renamo, Alphonso Dhlakama ambao utawaongezea uwezo wa utawala wa marais hao wawili.

 

MAPUTO, Msumbiji

RAIS Filipe Nyusi wa Msumbiji wiki iliyopita alitangaza mpango wa ugawanaji madaraka na Rais wa Renamo, Alphonso Dhlakama ambao utawaongezea uwezo wa utawala wa marais hao wawili.

Hakuna tangazo lililotolewa juu ya masuala ya kijeshi lakini Nyusi aliahidi kutoa taarifa zaidi hivi karibuni.

Kipengele muhimu katika mkataba huo kilikuwa ni kungezeka kwa nguvu za mabaraza ya majimbo na manispaa lakini akuna magavana wa kuchaguliwa na kuanzia mwaka huu 2018 iwe mwisho kwa meya waliochaguliwa.