http://www.swahilihub.com/image/view/-/4562254/medRes/1973267/-/92vfdn/-/abiy.jpg

 

Serikali Ethiopia yajadiliana na wapinzani wake

Dkt Abiy Ahmed

Waziri Mkuu wa Ethiopia Dkt Abiy Ahmed ambaye ameanzisha majadiliano na wapinzani. Picha/HISANI 

Na MASHIRIKA

Imepakiwa - Tuesday, May 15  2018 at  10:10

Kwa Muhtasari

Taarifa ya Oromo Democratic Front (ODF) iliyotolewa Mei 13, 2018, imethibitisha kwamba ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ya Ethiopia ulikutana na viongozi wao na wakafanya majadiliano yaliyozaa matunda kuanzia Mei 11 hadi Mei 12.

 

ADDIS ABABA, Ethiopia

SERIKALI ya Ethiopia imeanzisha rasmi mazungumzo kuhusu mageuzi ya kisiasa kwa kushirikisha kundi la upinzani lililoko uhamishoni la Oromo Democratic Front (ODF).

Taarifa ya ODF iliyotolewa Mei 13 imethibitisha kwamba ujumbe wa ngazi ya juu wa serikali ulikutana na viongozi wao na wakafanya majadiliano yaliyozaa matunda kuanzia Mei 11 hadi Mei 12.

“Kwa kuzingatia msimamo wetu wa muda mrefu, ODF ilisisitiza dhamira yake ya kuongeza na kupanua mchakato wa mageuzi na demokrasia,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

ODF hawakutaja ni maofisa gani wa serikali walikuwa katika ujumbe huo lakini waliongeza kwamba serikali ilikubali kwamba iko tayari kushiriki katika juhudi zote zisizo za vurugu.

ODF ilisema kwamba hata hivyo ilikuwa hatua chanya na kwamba bado kuna mengi zaidi yanahitajika kufanyika. “Pande zote mbili zilitilia mkazo kwamba majadiliano haya na ODF ni mwanzo wa ushirikishwaji mpana zaidi,” walisisitiza.

Taarifa ilisema kwamba chama kilikuwa tayari na shauku ya kuchukua jukumu la kuwezesha wadau wote kufanya mageuzi ambayo lazima yaongoze kuwa na mjadala wa pamoja katika kuelekea kwenye upatanisho wa kitaifa na maridhiano.

Walisema pia kwamba wajumbe watarejea nyumbani wakiwa na mpango wa kuanzisha mchakato kusajili chama cha siasa.