http://www.swahilihub.com/image/view/-/4022034/medRes/1706034/-/5b8ff6/-/nae.jpg

 

Serikali ya Marekani huenda ikafungwa leo

Donald J. Trump

Rais wa Marekani, Donald J. Trump. Picha/HISANI 

Na MWANDISHI WETU

Imepakiwa - Friday, February 9  2018 at  10:09

Kwa Mukhtasari

Bunge la Marekani kwa mara nyingine limekumbwa na mvutano juu ya kuongeza muda wa matumizi ya Serikali huku kukiwa na wasiwasi wa mvutano kukosa ufumbuzi hivyo kufanya shughuli za Serikali kufungwa.

 

WASHINGTON DC, Marekani

BUNGE la Marekani kwa mara nyingine limekumbwa na mvutano juu ya kuongeza muda wa matumizi ya Serikali huku kukiwa na wasiwasi wa mvutano kukosa ufumbuzi hivyo kufanya shughuli za Serikali kufungwa.

Alhamisi usiku ilikuwa siku ya mwisho kwa Bunge hilo kumaliza mvutano huo na kukiwa na dalili pande zinazovutana kushindwa kumaliza tofauti zao.

Ingawa wabunge wa Baraza la Wawakilishi wameidhinisha mswada wa bajeti ya muda mapema wiki hii kutokana na vyama vyao lakini kazi kubwa ilibaki kwa Baraza la Seneti ambalo kura 60 zilihitajika kuidhinsha mswada huo.

Wabunge 245 wa Chama cha Republican walipitisha mswada wa matumizi ya Serikali huku wa Democrats wakipinga kwa kura 182 ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Rais Donald Trump kusema angependa kuona Serikali kuu imefungwa.

Rais Trump na chama chake wanataka mageuzi ya uhamiaji yaambatanishwe na kuidhinishwa kwa bajeti ya mwaka 2018.