http://www.swahilihub.com/image/view/-/2629754/medRes/950439/-/45nyg5/-/TFRAY1902.jpg

 

Taarifa kuhusu Ray C zamkasirisha Jakaya Kikwete

Rehema Chalamila al-maarufu Ray C

Msanii mahiri wa Bongo Flava, Rehema Chalamila al-maarufu Ray C akiwa afisini katika wakfu alioanzisha wa kuwanufaisha vijana walioathirwa na mihadarati. Picha/HENRIETTA 

Na THOMAS MATIKO

Imepakiwa - Thursday, April 14  2016 at  15:29

Kwa Muhtasari

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete sasa kakasirika na taarifa kwamba mwanamuziki Ray C karejea tena kulamba unga.

 

RAIS mstaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete sasa kakasirika na taarifa kwamba mwanamuziki Ray C karejea tena kulamba unga.

Itakumbukwa kwamba kiongozi huyu ndiye alimkomboa Ray C kipindi akiwa anakaribia mauti na kumpeleka rehab hatua iliyomsaidia na kumfanya mwanamuziki huyo arejee kwenye hali ya akili razini.

Kwa kipindi cha miaka mitatu Ray C amekuwa katika tiba ya Methadone mpango ambao Kikwete alihakikisha unatekelezwa ili kumkomboa lakini ni kama vile msanii huyu aliyefifia, kajisahau tena na kurejelea uraibu huo hatari wa ulambaji poda.

Magazeti ya Bongo yakekuwa yakiripoti kwamba anachokifanya Ray C siku hizi ni kuchanganya tiba ya meth na unga huku akiendelea kudai kwamba hatumii mihadarati hiyo.

Sasa kiongozi huyo anaripotiwa kumwonya Ray C kuhusu kutokuzingatia matumizi ya meth.

Mwananyamala

Kwa mujibu wa chanzo kimoja katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam anakopokea tiba hiyo, Ray C alipata onyo hilo baada ya magazeti ya Global kuandika kwamba nyota huyo amerejea kwenye kubwia unga huku akiendelea na methadone, hali ‘inayomzimisha’ mara kwa mara.

“Jamani nataka kuwaambia, mnajua mlipoandika kwamba Ray C karejea kwenye unga wakati akiendelea kutumia methadone, JK (Jakaya Kikwete) alisoma, akamtumia ujumbe akimtaka ajiangalie kwenye kukazana kutumia dawa na kuachana moja kwa moja na matumizi ya unga. JK amemtaka aangalie mwenendo wake kwa sasa. Yaani bwana sijui vipi, JK anamtakia mema lakini yeye hajijui tu,” chanzo hicho kilinukuliwa.