http://www.swahilihub.com/image/view/-/4369558/medRes/1927556/-/12v66ab/-/tshisekedi.jpg

 

Ushindi wa Tshisekedi waungwa mkono

Mwanawe Tshisekedi ateuliwa kuwania urais DRC

Felix Tshisekedi. Picha/MAKTABA 

Na CHARLES WASONGA

Imepakiwa - Wednesday, January 30  2019 at  10:28

Kwa Muhtasari

Ushindi wa Tshisekedi licha ya kutoungwa mkono na baadhi ya mataifa, umeweka historia mpya DRC.

 

KINSHASA, DRC

VIONGOZI watatu wa kundi la waasi akiwamo mmoja aliyechinja polisi 40 wamejisalimisha na kumuunga mkono Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi.

Watu wote hao wametoka kwenye kundi la waasi linaloongozwa na Kamwina Nsapu (Black Ant) linalotuhumiwa kumwaga damu za watu wengi nchini humo.

Viongozi hao wamewaamuru wapiganaji wake kuweka silaha chini na kumuunga mkono Rais Tshisekedi.

Kundi jingine lenye waasi zaidi ya 600 kutoka Kasai nalo walikubali kuweka silaha zao chini baada ya kiongozi huyo wa nchi kuapishwa.

Lokondo Luakatebua, miongoni mwa viongozi wa waasi hao alituhumiwa kuliongoza kundi hilo mwaka 2017 na kuua askari 40 eneo la Luebo.

Akielezea kuhusu waasi hao kuunga mkono Serikali kiongozi wa mji wa Luebo, Joseph Mutshipayi alisema kwamba viongozi hao wamejisalimisha wakitokea msituni na askari wao 60.

“Walitupatia bunduki nne za AK 47 huku wakisema wapo tayari kufanya kazi na Serikali,” alisema.

Alisema kwamba wengine wamekabidhi risasi hizo maeneo mengine zikiwa nyingi ni za jadi katika mji wa Tshikapa.

Rais Tshisekedi aliapishwa wiki iliyopita na kuwa rais mpya wa DRC, akichukua nafasi ya aliyekuwa mtangulizi wake Joseph Kabila.

Uchaguzi huo ulifanyika kwa amani ikiwa ni historia kwa nchi hiyo kukabidhiana madaraka bila umwagikaji wa damu tangu ipate uhuru kutoka utawala wa Ubelgiji.

Baadhi ya nchi za Magharibi zagoma kutuma pongezi

Nchi za Magharibi hazikumtumia pongezi Tshisekedi na Ufaransa imeeleza wasiwasi wake juu ya matokeo rasmi ya uchaguzi, ambayo yalimpatia ushindi Tshisekedi kwa asilimia 38.57 ya kura zote zilopigwa na Fayulu kupata asilimia 34.8.

Kuthibitisha

Gazeti la Financial Times na vyombo vingine vya habari vya kimataifa vilithibitisha kuona nyaraka zinazosema kuwa mpinzani, Martin Fayulu ndiye mshindi wa uchaguzi huo.

Kambi ya Fayulu iliusifu Umoja wa Afrika kwa kutoa ombi la kutaka matokeo ya mwisho yaahirishwe, lakini kambi ya Tshisekedi halikufurahishwa.

Mvutano huo umezua wasiwasi kwamba mgogoro wa kisiasa ulioanza mara baada ya Rais Kabila kukataa kuachia madaraka mwishoni mwa muhula anaoruhusiwa kikatiba kumalizika miaka miwili iliyopita unaweza kusababisha umwagaji damu.